Monday, June 25, 2012

WAWILI WAFARIKI KATIKA MATUKIO TOFAUTI DAR

Na mwandishi wetu

Watu wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti yaliyotokea jijini Dar es Salaam likiwemo la mtoto mdogo kuuungua na moto.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marieta Komba, alisema tukio hilo limetokea Juni 23 mwaka huu, saa tano usiku eneo la Kigogo kwa Msafa, ambapo moto huo ulizuka ghafla katika nyumba ya Bw. Ramadhani Ramadhani.


Alisema nyumba hiyo yenye vyumba vinne, kimoja ndio kiliteketea kwa moto wakati marehemu Ramadhani akiwa amelala na dada yake Maria Ramadhani ambaye alipata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na kukimbizwa katika Zanahati ya Pugu Kajiungeni.

Kamanda Komba alisema, chanzo cha moto huo ni kibatari kilicholipuka na kushika godoro wakati mama yao akiwa katika ngoma ya unyago iliyokuwa ikifanyika jirani na nyumba yao.

Aliongeza kuwa, moto huo ulizimwa na wakazi wa eneo, maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Katika tukio jingine, gari isiyojulikana namba zake jana alfajiri ilimgonga mtembea kwa miguu katika Barabara ya Kilwa, eneo la Mtoni Mtongani, wilayani Temeke.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, David Misime, imesema marehemu alikuwa akitembea bila nguo ambapo umri wake unakadiriwa kuwa miaka 28-30, ambaye alifariki papo hapo na dereva kukimbia na gari yake.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke na juhudi za kulisaka gari na dereva zinaendelea.



 




No comments:

Post a Comment