Wednesday, June 20, 2012

FM ACADEMIA KUFANYA MAKAMUZI ARCADE


BENDI ya muziki wa dansi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma', wanatarajia kufanya onesho lililopewa jina la ‘Usiku wa Windhoek na Ngwasuma’, ambalo litafanyika keshokutwa katika Ukumbi wa Arcade, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Katika onesho hilo, watu 100 wa kwanza watapata bia moja bure ili kuwafanya wafurahie muziki wa bendi hiyo utakaokuwa unaporomoshwa ukumbini hapo.

Akizungumza Dar es Salaam  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga alisema mashabiki watapata burudani ya nguvu kutoka kwao, hivyo ni wakati wao kuingia kwa wingi kushuhudia onesho hilo.

Alisema FM Academia ni bendi imara yenye mashabiki lukuki, hivyo wanaamini watafurahia burudani itakayoporomoshwa na bendi hiyo chini Rais wake Nyoshi el Saadat.

“Mashabiki wetu waje kwa wingi katika shoo yetu ili wapate burudani ya nguvu itakayopambwa na nyimbo zetu mpya na zile za zamani ambazo zipo kwenye kiwango cha juu.

“Naamini mambo yatakuwa mazuri, ukizingatia kwamba wanamuziki wetu wamejipanga imara kuwapatia vitu vya hali ya juu, ili kuiweka juu bendi,” alisema.




No comments:

Post a Comment