Tuesday, March 06, 2018

MAMA KIKWETE MGENI RASMI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI TABORA

Picha ya Mtandao
NA TIGANYA VINCENT
TABORA
Mke wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete (pichani kulia)anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa Mkoa wa Tabora.

Maadhimisho hayo mwaka huu kimkoa yanatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Chipukizi katika Manispaa ya Tabora na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora Queen Mlozi alisema katika maadhimisho hayo wakinamama wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbalimbali mkoani humo watapata fursa ya kuonyesha kazi mbalimbali wanazoshughulika nazo katika kujiletea maendeleo.

Aliongeza kuwa jioni kutakuwepo na Chakula(dinner) ambapo kila mshiriki anatakiwa kuchangia fedha na kuongeza kuwa kutakuwepo na burudani kutoka kwa wasanii wakubwa akiwemo Hadiha Kopa.

No comments:

Post a Comment