Wednesday, February 28, 2018

SERIKALI YAAHIDI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI MNADA PUGU, YASIMAMISHA UJENZI NYUMBA MPYA


PICHANI: Waziri wa Mifugo na Uvuvi Kuhaga Mpina akizungumza na wananchi katika Mnada wa Pugu, Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema.

Na Bashir Nkoromo, Pugu

Serikali ameagiza shughuli mpya za ujenzi na nyingine za maendeleo ikiwemo kilimo katika Kijiji cha Bangulo Kata ya Pugu Stesheni kusimama kuanzia leo, kusubiri mgogoro wa eneo kati ya Kijiji hicho na Mnada wa mifugo wa Pugu upatiwe ufumbuzi.

Akizungumza na wananchi leo baada ya kutembelea maeneo ya mpaka wa Mnada huo, Waziri wa Mifugo na Uvivi Luhaga Mpina ametoa agizo hilo kunusuru hali ya fukuto la mapigano katika ya wafanyabiashara kwenye mnada huo kudai Wanakijiji hicho cha Bangulo kuvamia eneo la malisho.

"Baadhi yenu mmeonyesha hapa hati za kumiliki makazi, lakini pia tunafahamu kuwa eneo la Mnada lilikuwa na ukubwa wa ekari 190, hivi sasa limebaki eneo kama asilimia 20 tu ya malisho. Hali hii inaufanya Mnada huu kukosa sifa, hivyo wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa kudumu naagiza shughuli zote za ujenzi na kilimo zisimame kwanza kuanzia leo," alisema Mpina.

Waziri Mpina amewataka wananchi kuishi bila hofu akisema suala lao litapatiwa ufumbuzi ambao utakuwa wa kudumu.

Habari katika PichaSehemu ya eneo la Mnada wa Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, leo


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimkaribisha kufanya ziara, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina alipowasili kwenye Mnada wa Pugu wilayani hummo, Dar es Salaam, leo


Waziri Mpina akimsalimia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alipowasili kwenye Mnada wa Pugu leo


Waziri Mpina akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kabla ya kuanza ziara


Sohia Mjema akimuongoza Waziri Mpina kwenye eneo la kufanya mazungumzo na uongozi wa Mnada huo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo


Mkuu wa Mnada wa Pugu Kevamba Samwel akizungumzia hali ya maendeleo na changamoto za Mnada huoMatibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo akijibu baadhi ya changamoto zilizoelezwa na mkuu wa Mnada huoMkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akieleza anavyozijua na alivoanza kuzishughulia baadhi ya changamoto za Mnada huo hasa mgogoro wa arhi baina ya Mnada na Wananchi"Naona mda unakwenda mbio, hebu tuanze utembeleaji mipaka..." akasema waziri Mpina huku akitazama saa yakeWaziri Mpina akijadiliana na Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema kipi waanze kati ya kuzungumza kwanza na wananchi au kukagua mipakaKatibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Maria Mashungo akiwa ameweka bakora begani wakati safari ya kukagua mipaka ikianza. Kushoto ni Katubu wa Mwenezi tawi la CCM Bangulo Kata ya Pugu Stesheni Loyce HamisiWaziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (kushoto) akiongoza kupanda moja ya vilima vilivyo katika Kijiji cha Bangulo wakati akikagua mipaka ya kijiji hicho na Mnada wa Pugu leoMkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema naye akijiandaa kupanda kilima hicho"Kwa hiyo hadi kulee ni eneo la malisho ya Mnada?" Waziri Mpina akiuliza maofisa aliofuatana nao. Wapili kushoto ni DC MjemaAfisa wa Mnada akimpatia maelezo waziri Mpina kuhusu lilivyo eneo la malisho ya Mnada wa PuguKamanda wa Polisi wilaya ya Ilala Kamishna Msaidizi Salim Hamduni akiongoza msafara wakati wa kushuka baada ya Waziri Mpina kukagua badhi ya maeneo ya mipaka kati ya kijiji cha Bangulo na Mnada wa PuguKisha waziri Mpina naye akashuka kilima hichoKatibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri Mpina baada ya kutoka kukagua mipaka hiyoKatibu Tawala wa Wilaya ya Ilala edward Mpogolo (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri Mpina baada ya kutoka kukagua mipaka hiyoBaadhi ya nyumba katika kijiji cha Bangilo kinachodaiwa kuvamia eneo la malisho ya Mnada wa Pugu. Kushoto ni Waziri Mpina"Wenyewe mpo?" Waziri Mpina akiuliza huku akichungulia kwenye geti la nyumba moja inayoonyesha kujengwa hivi karibuni ambayo inadaiwa kuwa miongoni mwa nyumba za wananchi wa kijiji cha Bangulo waliovamia eneo la malisho la Mnada wa Pugu.Aloyce Malya mkazi wa Kijiji cha Bangulo akizungumza wakati waziri Mpina alipozungumza na wananchi kuhusu mgogoro wa ardhi baina ya wanankijiji hicho na Mnada wa Pugu leoKisha Aloyce akatia hati yake ya umiliki wa ardhi na kumkabidhi waziri MpinaWaziri Mpina akiipitia kwa makini hati hiyo baada ya kuipokeaHati yenyewe kwa karibuWaziri Mpina akizungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo mgogoro wa mipaka kati ya wananchi na Mnada wa PuguWananchi wakimsikiliza waziri MpinaWaziri Mpina akiwaaga baada ya mazungumzo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment