Friday, October 06, 2017

MBUNGE WA MAFINGA MJINI AKABIDHI MIFUKO 130 YA SARUJI


PICHANI: Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya kuchochea maendeleo na kama unavyo muona akiwa anashusha safuji hiyo kutoka kwenye gari


Na Fredy Mgunda,
Iringa

Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji 130 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maarifa,kinyanmbo na zahanati ya Rungemba kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa lengo la kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kuel kuhakikisha natimiza azma yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini.

“Nimetoa mifuko 130 ya saruji kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi wa madarasa katika shule mpya ya Maarifa na zahati ya Rungemba hii ni mwamzo tu nitaendelea kutoa saruji nyingine ili kulifanya jimbo la Mafinga Mjini kupata maendeleo kwa kasi” alisema Chumi
Chumi alisema kuwa halmashauri ya Mji wa Mafinga imeshaanda mpango kabambe ambao utakuwa msaada mkubwa kuchochoe maendeleo kwa kasi huku mji ukiwa umeshapangiliwa jinsi gani ya kuitumia vizuri ardhi ya halmashauri hii.

“Ukiangalia miji mingi inakuwa bila kuwa na mpango kabambe kitu kinachokuja kusababisha migogoro ya kugombea ardhi hivyo mpango huu utakuwa namanufaa makubwa kwa jimbo hili la Mafinga Mjini” alisema Chumi

Aidha Chumi alisema kuwa shule zilipata saruji hiyo ni shule mpya ya Maarifa nimekabidhiwa mifuko 50 ya saruji sawa na nyingine ya Kinyanambo lakini pia nimetoa mifuko ya saruji 30 kwa zahanati ya Rungemba lengo ni kuchochoe kuleta maendeleo kwa wananchi.

Chumi amewapongeza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kata za ametoa ahadi ya kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa shule zote za jimbo la mafinga mjini.

Naye mwenyekiti kata ya Changalawe Emmanuel Kuzugali ameelezea jinsi wananchi walivyochangia kuwezesha ujenzi wa shule ya msingi utakaoanzishwa katika kata hiyo.

Kwa upande wake diwani viti maalumu kata ya changalawe Monica Luvanda ameelezea mchakato ulivyokuwa hadi kupelekea kushirikiana na wananchi kuanzisha ujenzi wa shule ili kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa kata hiyo.


Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji akiteta jambo na wananchi waliofika katika eneo hilo alipokuwa akikabidhi saruji hizo.







No comments:

Post a Comment