Saturday, September 09, 2017
POLEPOLE AFURAHISHWA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI PSPF
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (kushoto), akimkabidhi fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), na vipeperushi mbalimbali vyenye taarifa za kina kuhusu huduma zitolewazo na Mfuko huo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Bw. Humphrey Polepole, wakati alipotembelea banda la Mfuko kwenye maonesho yaliyoambatana na Tamasha la Jinsia 2017, lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania, (TGNP), kwenye viwanja vya Mtandao huo Mabibo jijini Dar es Salaam, Septemba 8, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Bw. Humphrey Polepole,(pichani juu), amefurahishwa na mpango wa uchangiaji wa hiari wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutokana na faida azipatazo mwananchama hususan bima ya Afya.
Bw. Polepole alionyesha kuridhishwa kwake na mpango huo ujulikanao kama PSS, baada ya kupatiwa maelezo kuhusu faida mbalimbali azipatazo mwanachama, wakati alipotembelea banda la PSPF kwenye maonesho yaliyoambatana na Tamasha la Jinsia 2017, lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania, (TGNP), kwenye viwanja vya Mtandao huo, Mabibo jijini Dar es Salaam, Septemba 8, 2017.
“Mpango huu ni mzuri kwani serikali ya CCM iliwaahidi watanzania kuwapatia huduma ya afya ambayo itawafikia watanzania wote na mimi ninaamini kwa viwango mlivyonitajia watanzania wengi wanaweza kumudu kuwa na bima ya afya,” alifafanua Bw. Polepole.
Alisema yeye yuko tayari kushirikiana na PSPF katika kuwapatia elimu wana CCM na wananchi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mpango huo. “Mimi tayari ninayo bima ya afya, lakini niko tayari kuhamasisha wananchi ili waweze kujiunga na mpango huu kwani ni mzuri, na kinachohitajika ni elimu kuwafikia ili waelewe umuhimu wake.” Alifafanua Bw. Polepole.
Akimpatia maelezo kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na PSPF, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw Abdul Njaidi alisema, Mpango wa uchangiaji wa hiari umelenga makundi mbalimbali ya wananchi wenye shughuli inayowapatia kipato kama vile, madereva wa bodaboda, mama lishe, machinga na wajasiriamali wengine.
“Kujiunga na mpango huu ni bure, na mwananchi aliyejiunga na mpango huu atapaswa kuchangia kiasi cha fedha kisichopungua shilingi elfu 10,000/= kila mwezi, lakini jambo la muhimu zaidi, pamoja na kufaidi mafao mablimbali, mwanachama pia atakuwa na fursa ya kujiunga na bima ya afya,” alifafanua Bw. Njaidi.
Naye Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF Bw. Delphin Richard, akifafanua zaidi alisema, mpango wa PSS umekuwa na faida kubwa kwa wananchi ambao wengi wamekuwa wakihitaji kupatiwa bima ya afya.
“Muitikio wa wananchi kujiunga na PSS umekuwa mzuri kwani wengi wao huhitaji kupatiwa bima ya afya kwa hivyo sisi kama PSPF tunawahamasihsa wananchi kutumia fursa hii ya kujiunga na PSS kwani ukiacha fao hilo la afya kuna mafao mengine kama mikopo ya elimu, viwanja na nyumba.” Alifafanua Bw. Delphin.
Kando na Bw. Polepole kutembelea banda la PSPF, pia Wananchi mbalimbali waliweza kufika kwenye banda hilo kupatiwa elimu kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PSPF, miongoni mwa waliofika ni Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi, ambaye naye aliahidi kuwaunganisha wanachama wa Mtandao huo ili waweze kukutana na maafisa wa PSPF kuwapatia elimu kuhusu umuhimu na faida za kujiunga na PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari.Kongamano hilo lililozinduliwa na Makamu wa Rais, Mhe.Samia Suluhu Hassan Septemba 5, 2017, limefikia kilele Ijumaa Septemba 8, 2017,.
Bw. Polepole, (kulia), akimsikilzia kwa makini, Bw. Njaidi.
Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PSPF Bw. Delphin Richard, (kushoto), akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu huduma zitolewazo na PSPF, kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Bw. Humphrey Polepole.
Afisa Msaidizi wa PSPF, Bw. Win-God Mushi, (kulia), akimpatia maelezo, Bi Agness G. Lukanga aliyetembelea banda la PSPF na kisha kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS)
Afisa Msaidizi wa PSPF, Bw. Win-God Mushi, (kulia), akiwapatia maelezo, waanchi hawa waliotembelea banda la Mfuko huo.
Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF Bw. Delphin Richard, (kushoto), akimpatia maeelzo, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi, alipotembelea banda la Mfuko huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi.
Bw. Polepole, (kulia), akizungumza mbele ya Bw. Njaidi ambapo alitoa ushauri mbalimbali na kuahidi kusaidia kuhamasisha wana CCM na wananchi kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari PSS.
Mama huyu akijaza fomu za kujiunga na Mpango wa PSS.
Mama huyu akipigwa picha ya kitambulisho cha uanachama wa PSPF, kupitia Mpango wa PSS, ambapo mwanachama hupatiwa kitambulisho punde tu anapojiunga.
Mama huyu akipigwa picha ili kupatiwa kitambulisho cha uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa PSS.
Bw. Delphin, (kulia), akimpatia vipeperushi vya PSPF mama huyu aiyetembelea banda la Mfuko huo.
Bw. Delphin, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na PSPF, Bi.Agness G. Lukanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment