Saturday, September 16, 2017

MWILI WA MAREHEMU SISTER JEAN PRUITT KUAGWA JUMATANO


Ndugu, jamaa, marafiki na wadau wa sanaa na haki za watoto Tanzania.

Kamati ya Maandalizi ya Msiba inapenda kutoa Tangazo rasmi la shughuli ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mpendwa wetu marehemu Sister Jean Pruitt itakayofanyika siku ya Jumatano tarehe 20/09/2017.

Shughuli hii itafanyika katika Ukumbi wa Karimjee uliopo Posta, Mtaa wa Sokoine, mkabala jijini Dar es salaam. Wadau wote tunaombwa kuwasili mapema kwa ajili ya kutoa heshima zetu za mwisho na kuaga mwili saa 3:30 asubuhi siku hiyo.

Baada ya hapo Mwili utasindikizwa kwenda kanisa la Mt. Joseph kwa ajili ya misa itakayoanza saa 9 Alasiri siku hiyo ya Jumatano.

Tunawaomba tuzidi kumwombea mama yetu Sista Jean Pruitt apumzike kwa Amani. 
Raha ya milele umpe eh Bwana na mwanga wa milele umwangazie,

Apumzike kwa Amani - Amina

Kamati ya Maandalizi ya Msiba



No comments:

Post a Comment