Thursday, August 31, 2017

SABABU YA EID-AL-ADHA KUITWA 'SIKUKUU YA KUCHINJA'


Na Jumia Travel Tanzania

Eid al-Adha ni miongoni mwa sikukuu kubwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu ukiachana na Eid- al-Fitr inayosherehekewa kila mwaka duniani kote. Kwa mwaka huu sikukuu hii inatarajiwa kusherehekewa siku ya Ijumaa ya Septemba mosi ambapo kwa waumini wa dini hiyo ni kipindi cha kujitolea, kuonyesha ukarimu kwa marafiki, familia na watu wenye uhitaji.

Kama zilivyo sikukuu nyingine kuna baadhi ya watu huwa hawajui ni kwa nini huwa zinaseherehekewa namna zinavyosherehekewa. Jumia Travel kupitia makala haya imekukusanyia mambo ya msingi kuhusu maana ya sikukuu hii na namna ya kusherehekea.

Waislamu huisherekea sikukuu ya Eid al-Adha kwa kuchinja mnyama ikiwa ni kuheshimu kitendo alichokifanya Ibrahim au Abraham (anavyoitwa na Wakristu na Wayahudi). Ibrahim aliamriwa na Mungu kumtoa mtoto wake pekee kiume kama sadaka kwa kumchinja ambapo alikubali kutii amri hiyo bila ya kupinga. Kabla ya kumtoa sadaka mtoto wake sadaka, Mungu aliingilia kati kwa kumtuma Malaika wake ambaye altaka amchinje kondoo badala ya mtoto wake.
Katika kuadhimisha tukio hilo kubwa la kiimani, kila mwaka sikukuu hii inaposherehekewa waumini wa Kiislamu huchinja mnyama halali kwa mujibu wa imani. Mnyama huyo anaweza kuwa ni ng’ombe, ngamia, mbuzi au kondoo inategemea na uwezo wa mtu. Baada ya kuchinja, nyama hugawanywa katika mafungu matatu ambapo la kwanza hubakia kwa familia; la pili hugawiwa kwa ndugu, jamaa na marafiki; na kisha la tatu hugawiwa kwa watu masikini na wenye uhitaji.

MAMIA WAMIMINIKA KUJISAJILI MFUKO WA FIDIA (WCF)


Meneja Matekelezo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena, (kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na kulipa michango leo Agosti 31, 2017.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MUITIKIO wa waajiri kujisajili na kulipa michango katika Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa wa kuridhisha hususani Mwezi Agosti, Meneja Matekelezo Bw. Victor Luvena amesema leo Agosti 31, 2017.

Itakumbukwa ya kwamba, tarehe 23 Julai 2017 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), alitoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao walikuwa hawajasajili kuhakikisha wanajisajili katika Mfuko na wanawasilisha michango kwa wakati, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao na kama Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi inavyoelekeza.

RAIS AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA ULINZI NA USALAMA WA SASA NA WASTAAFU IKULU, DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika chumba cha mkutano kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakaribisha viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa sasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2017


POLEPOLE: TUPO TAYARI KWA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA LONGIDO

Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Chama cha Mapinduzi kimesema kuwa kipo tayari kuingia katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Longido Mkoani Arusha mara baada ya kutangazwa kuwa jimbo hilo lipo wazi kutokana na maamuzi ya mahakama ya Rufaa iliyobainisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2015 haukuwa huru na haki hivyo kufuta matokeo ya uchaguzi huo.

CCM imeeleza kuwa kulikuwa na matumizi yasiyostahili kutumika kujazwa matokeo ya Ubunge, kwa kutumia fomu namba 21c za kujaza matokeo ya Udiwani na kujaza matokeo ya Ubunge, badala ya kutumia fomu namba 21b jambo lililopelekea kufungua kesi ya kupinga ushindi wa Ubunge katika Jimbo hilo.

Kauli ya CCM imetolewa na Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Polepole alisema kuwa vipo vyama vya siasa ambavyo kwa kawaida hulalamika kila vinaposikia kushindwa na mahakama kwa madai kuwa hakuna haki lakini vyama hivyo kila vinaposhinda vyenyewe husema mahakama imetenda haki.


NIC BANK YAKABIDHI MAGARI MATATU KATI YA SITA KWA MTEJA WAKE KAMA MKOPO


Meneja mahusiano kwa wateja wakubwa wa benki ya NIC Tanzania, Woinde Murro(kulia) akizungumza jambo na mmoja wa wateja waliofika kwaajili ya kukabidhiwa magari makubwa ikiwa awamu ya kwanza ya mkopo wa Magari Sita ambapo leo amepokea magari matatu na matela matatu


Leo benki ya NIC imekabidhi magari makubwa matatu na matela yake kati ya magari sita ambayo yamekabidhiwa kama mkopo kwa Mteja wao Simera. Makabidhiano ya Magari hayo yamefanyika katika Ofisi za FAW zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw.Zainul Dossa amepokea magari hayo kati ya sita waliyokopeshwa na Benki ya NIC mapema leo huku magari mengine matatu yatakabidhiwa hivi karibuni.

Meneja mahusiano kwa wateja wakubwa wa benki ya NIC Tanzania, Woinde Murro(kulia) akimkabidhi funguo Mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Simeta, Bw.Zainul Dossa(kushoto) za magari matatu waliyokopeshwa na Benki ya NIC


TMA YAWAJENGEA UWEZO WANAHABARI KUHUSU HABARI ZA HALI YA HEWA


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (kulia) akizungumza alipokuwa akifungua semina ya kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Wengine kutoka kulia ni Bi. Mariam Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa TMA na Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa.[ Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (kulia) akizungumza alipokuwa akifungua semina ya kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Matumizi Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladslaus Chang'a , Meneja Ofisi Kuu ya Utabiri, Samwel Mbuya, pamoja na Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa.


MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini Tanzania leo imewapa semina baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi alisema semina hiyo ni utaratibu wa TMA kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuwa mabalozi wa zuri wa kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi mazuri ya taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na TMA kwa wananchi.


WASANII NGULI NCHINI KUPIMANA MABAVU DIMBA CONCERT TRAVELNTINE MAGOMENI

PICHANI: Meneja Tukio wa Tamasha la Dimba Concert , Mwani Nyangasa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Tamasha litakalo wakutanisha Wakongwe wa Muziki wa Dansi nchini na bendi ya Msondo Ngoma katika ukumbi wa Traventine September 2 mwaka huu kwa kiingili cha shilingi 10,000 na 20,000 kwa VIP.

Na Agness Francis,Globu ya Jamii

Wanamuziki wakongwe wa Muziki wa Dansi nchini wametambiana kuoneshana uwezo wa kuimba siku ya Tamasha la Dimba Concert litakalofanyika katika ukumbi wa Traventine Magomeni Septemba 2 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam meneja tukio tamasha la dimba concert,Mwani Nyangasa amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa Taifa muziki bendi kupambana na wanamuziki nguli wa Bendi ya Msondo ngoma.

“ dhumuni la tamasha hili ni kuendeleza muziki wa dansi hapa nchini kwa kutumia wasanii hawa wakongwe ili waweze kuonesha vijana,wapenzi na wadau kuwa muziki huu bado upo hai.” Amesema Nyangasa.


VIJANA WA JKT WACHANGIA DAMU NA KUFANYA USAFI


Takataka zikiondolewa.

Na Dotto Mwaibale

ASKARI wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi namba 831 KJ Mgulani, wamejitolea kuchangia damu pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho kutwa nchini kote.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali Zacharia Godfrey Kitani alisema kila maadhimisho hayo yanapofanyika wamekuwa wakifanya shughuli za kijamii kama kufanya usafi na mwaka huu wameona wafanye usafi na kuchangia damu katika hospitali hiyo ili kusaidia wananchi.

"Ni kawaida yetu katika kuadhimisha siku ya kuanzishwa jeshi letu sisi kama askari kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika maerneo tofauti tofauti kwa siku kadhaa leo hii tunafanya usafi katika Hospitali ya Temeke na kutoa damu na tutaendelea katika maeneo mengine hadi siku ya kilele cha maadhimisho haya hapo kesho kutwa" alisema Kitani.


ASKARI WANAWAKE JKT MGULANI WASAFISHA WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE


PICHANI: Mkuu wa Idara ya wanawake Wanajeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi 831 KJ Mgulani (Matron wa Kikosi), Kapteni Lamla Balama baada ya kuzungumza na wanahabari Dar es Salaam leo kuhusu shughuli ya usafi waliofanya katika Wodi ya Wazazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho nchini.


Na Dotto Mwaibale

ASKARI Wanawake wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi 831 KJ Mgulani, wamefanya usafi katika wodi ya wazazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo , Mkuu wa Idara ya wanawake Wanajeshi katika Kikosi hicho (Matron wa Kikosi), Kapteni Lamla Balama alisema hii ni mara yao ya kwanza kama idara kufanya usafi katika hospitali hiyo.

" Tumeona ni vizuri na sisi kushiriki kazi za kijamii kwa kufanya usafi katika Hospitali hii kwa kushirikiana na vijana wetu 45 na sisi askari wa kudumu 27 ikiwa ni moja ya shughuli ya kuadhimisha siku yetu hiyo muhimu jeshin" alisema Balama.

"Ni kawaida yetu katika kuadhimisha siku ya kuanzishwa jeshi letu sisi kama askari Alisema shughuli kama hiyo imekuwa ikifanyika katika Hospitali zote za Serikali Jijini Dar es Salaam ambazo ni Mwananyamala, Temeke na Amana kulingana na walivyojipanga askari kutoka vikosi tofauti.

Akizungumzia shughuli hizo za usafi na kuchangia damu zinazofanywa na askari hao kuanzia jana na kuendelea leo kwa askari hao kutoka idara ya wanawake kwa kufanya usafi katika wodi ya wazazi, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Husna Msangi aliwashukuru askari hao kwa kazi hiyo kubwa walioifanya katika hospitali hiyo.

Akielezea jana kuhusu utoaji wa damu waliochangia askari hao alisema utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto ya damu hospitalini hapo kutokana kuwa na mahitahi makubwa ya damu kwa wagonjwa.

Alisema mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni makubwa hivyo amewaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu ambao wataweza kupoteza maisha kwa kukosa damu.


Wednesday, August 30, 2017

UJUMBE WA CPC WAKUTANA NA MANGULA CHUO KIKUU CHA SIASA CHA MWALIMU NYERERE, KIBAHA



Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula (kulia) akiongoza mazungumzo baina yake na Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017


Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula akimkaribisha Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole.


RIPOTI SAUTI ZA WANANCHI: KUHUSU HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Wananchi wengi wanatumia vituo vya afya vya serikali na husubiri chini ya saa moja kumuona daktari

Wakati huo huo, wananchi 7 kati ya 10 wanasema changamoto ipo katika upatikaji wa dawa na vifaa tiba

30 Agosti 2017, Dar es Salaam: Wananchi wanapopata majeraha ama kuugua, 6 kati ya 10 (61%) huenda katika kituo cha afya cha serikali. Kiwango hiki kimeongezeka kutoka 45% mwaka 2014 na kubaki hivyo hivyo tangu mwaka 2016. Kwa kiasi kikubwa hii imesababishwa na kupungua kwa watu wanaojitibu wenyewe kwa kwenda kwenye maduka ya dawa (9%), maduka ya kawaida kupata dawa (7%), wasiofanya chochote (1%) au wanaotafuta aina nyingine za matibabu (5%). Takwimu zilizokusanywa toka mwaka 2014 zinaonesha kupungua kwa matumizi ya njia hizo. Idadi ya wananchi wanaotumia vituo binafsi, vya kanisa ama vya mashirika yasiyo ya kiserikali haijabadilika katika kipindi hiki (16% mwaka 2017).

Pamoja na ongezeko la idadi ya wagonjwa, utaratibu wa wananchi kusubiri kwa saa moja ama chini ya hapo ili kumuona daktari haujabadilika toka mwaka 2014. Wananchi 7 kati ya 10 (70%) walisubiri kwa saa moja ama chini ya hapo mwaka 2014 ukilinganisha na wananchi 3 kati ya 4 (76%) mwaka 2017. Hata hivyo, wagonjwa husubiri kwa saa moja ama chini ya hapo katika vituo binafsi, vya kanisa ama vya mashirika yasiyo ya kiserikali (88% walisubiri kwa muda huu) ukilinganisha na vituo vya serikali (74% walisubiri kwa saa moja ama chini ya hapo).

Tuesday, August 29, 2017

DR.MABODI: ATAKA MIRADI YA MAJIMBONI IWANUFAISHE WANANCHI


Kulia ni Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akimkabidhi vifaa mkulima Trekta ndogo ya mkono (Power tillers) aliyevaa fulana ya rangi ya njano na kofia na wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Zanzibar Nadir Abdul-Latif Yussuf aliyetoa vifaa hivyo kwa wananchi hao.
 
Baadhi ya wananchi na viongozi waliofika katika hafla fupi ya makabidhiano ya matrekta (Power tillers) mbili na mashine moja ya umeme wa jua(solar).


 
Na Is-haka Omar, Zanzibar.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka wabunge, wawakilishi na madiwani kuhakikisha miradi wanayopeleka majimboni inawanufaisha wananchi wote.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Mabodi wakati akikabidhi matrekta madogo ya mkono (Power tillers) mbili na mashine ya umeme wa solar moja kwa wakulima wa jimbo la Chaani zilizotolewa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Nadir Abdul-Latif Yussuf.

Dkt. Mabodi alisema ahadi zinazotekelezwa na viongozi mbali mbali wa majimbo nchini ni lazima ziwanufaishe wananchi wote ili kufikia malengo ya mapinduzi kwa vitendo. Alieleza kuwa vifaa hivyo vya kilimo vilivyotolewa na mwakilishi huyo vinatakiwa kutumiwa vizuri na wakulima ili visaidie shughuli za kilimo katika jimbo hilo.

Aidha Dkt. Mabodi aliwasisitiza viongozi na watendaji wapya waliochaguliwa katika uchaguzi unaoendelea hivi sasa ndani ya chama na jumuiya zake kufanya kazi za taasisi hiyo kwa bidii ili chama hicho kiweze kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.

TAMKO KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA

TAMKO LA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA TIBA YA ASILI YA MWAFRIKA


Ndugu wananchi,

Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yalianza rasmi mwaka 2003 baada ya Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika kuridhia kuwepo kwa sherehe hizo. Maadhimisho haya hufanyika katika nchi 46 za kanda ya Afrika ambazo ni wanachama wa Shirika la Afya Duniani tarehe 31/08 ya kila mwaka.

Ndugu wananchi,

Tanzania, inaadhimisha maadhimisho haya kwa malengo makuu manne. Kwanza Tanzania ina nia ya kufufua ari na kujenga heshima ya huduma za tiba asili ambazo historia inatuambia kuwa zimekuwa zikikandamizwa na kudharaulika. Kwa kiwango kikubwa ukoloni pamoja na ukoloni mambo leo umekuwa ukikandamiza tiba zetu za asili na kufanya Waafrika wenyewe kuzinyanyapaa tiba hizo. Hali hiyo imetufanya tuyumbe, tukose dira na mwelekeo katika suala zima la kuboresha Tiba Asili katika nchi yetu.

Pili kwa kupitia maadhimisho haya Serikali inawahamasisha Waganga wa Tiba Asili kujiepusha na migongano katika jamii kwa kutohusisha ushirikina na uchawi kama chanzo cha ugonjwa. Kuna taarifa na migongano mingi ya kutisha juu ya hili. Itakuwa jambo la busara kwa waganga wa tiba asili kupitia kwenye vyama vyao kupanga mikakati ya kudhibiti na kuondoa kabisa vitendo vibaya vinavyochafua taaluma yao.


RC TABORA ATAKA MAELEZO ALIYECHOMA MOTO CHUO CHA ARDH

Na Tiganya Vincent
RS-TABORA

SERIKALI Mkoa wa Tabora imeagiza kutafutwa na kuchukiwa hatua kali na kupata maelezo ya watu waliohusika na uchomaji moto katika maeneo ya Chuo cha Ardhi Tabora na kusababisha uharibifu mkubwa wa mistu asili na miti iliyokuwa imepandwa katika eneo hilo kama hatua za uhifadhi wa mazingira.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kukuta eneo la Chuo hicho likiwa limeungua na moto wakati wa ziara ya ya kukagua vitalu vya kuoteshea miti ikiwa ni maandilizi ya zoezi la upandaji wa miti.

Alisema kuwa haiwezekani wananchi wanajitoa kwa moyo kupanda miti katika kampeni inayoendelea kisha watu wachache wanaamua kuua miti na kuharibu mazingira.

Mwanri aliongeza kuwa inasikitisha kuona hata sehemu za Taasisi za umma kama hiyo zinaacha moto unaunguza miti na wakufunzi wapo, wanachuo wapo bila kuchukua hatua ya kuuzima na kuwasaka waliohusika.

Alisema kitendo kinaonyesha jinsi wao nao wanahusika kwa namna moja au nyingine katika kuchangia uharibifu ulifanyika katika Chuo chako.

Kufuatia kitecho hicho Mkuu wa Mkoa alimwagiza Afisa Mazingira wa Manispaa ya Tabora kwenda kwa Mkuu wa Chuo kupata maelezo nini kilitokea na hatua zilizochukuliwa kwa wahusika na kama hawachukua hatua kwa wahusika basi Sheria za Mazingira zichukue mkondo wake.


TANROADS TABORA KUTEKELEZA AGIZO LA JPM UJENZI WA BARABARA ZILIBAKI

Na Tiganya Vincent
RS-TABORA

WAKALA wa Barabara nchini (TANROADS) mkoani Tabora imesama kuwa tayari imeshaanza kutekeza hatua mbalimbali za maandalizi ya ujenzi wa barabara ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza ujenzi wake uanze mara moka wakati akiwa katika ziara ya mkoa huo.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Tabora na Meneja wa TANROADS Mhandisi Damian Ndabalinze kwenye kikao kazi kiliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa Mameneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini Tanzania(TARURA) wa mkoani humo.

Mhandisi Ndabalinze alisema kuwa katika barabara ya kutoka Kaliua hadi Urambo kazi za awali za kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi inaendelea katika eneo la mradi.

Monday, August 28, 2017

HIZI NDIO MECHI KUBWA ZA WATANI WA JADI BARANI AFRIKA


Na Jumia Travel Tanzania

Miongoni mwa matukio yanayosisimua zaidi kwenye mchezo wa soka ni mipambano ya watani wa jadi. Katika nchi nyingi barani Afrika ukiwauliza kwa harakaharaka mashabiki wengi wa soka ni mechi zipi huwa wanazisubiria sana utawasikia wanakutajia michezo kama vile Real Madrid na Barcelona, Manchester United na Manchester City, Inter Milan na AC Milan, Liverpool na Manchester United, Chelsea na Arsenal au Bayern Munich na Borussia Dortmund.

Kutokana na umaarufu wa soka la nchi za Ulaya imekuwa ni rahisi kwa mechi zao kufuatiliwa kwa urahisi ukilinganisha na huku Afrika. Lakini hiyo haimaanishi kwamba bara la Afrika nalo halina michezo ya namna hiyo ambayo ikiwa inakaribia homa miongoni mwa mashabiki huwa juu kuliko kawaida.

Saturday, August 26, 2017

BRG GEN. MBUNGU AWATAKA SUMA JKT GUARD KUWA MABALOZI WAZURI WA MAPAMBANO YA RUSHWA KAZINI



Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu akizungumza na askari wa ulinzi binafsi wa kampuni ya Suma JKT wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya sita kwa askari wapya wa kampuni hiyo iliyopo chini ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT). na kuwaasa kuwa mabalozi wazuri katika mapambano ya rushwa katika kazi yao na hasa katika ofisi watakazopangiw akufanya kazi



Mkurugenzi wa kampuni ya Ulinzi ya Suma Jkt Guard Limited, Meja Alfred Mwaijande akizungumza kabla ya kukamribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mafunzo ya askari wa kundila sita wa Suma jkt


DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam Agosti 25, 2017. Wahandisi wanawake wa TANESCO walikabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais, baada ya kuibuka wa kwanza kwenye kongamano na maonesho linalowakutanisha wahandisi wanawake kutoka sekta mbalimbali hapa nchini lijulikanalo kama "Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition-TW=AWECE". Wahandisi hao walionesha umahiri mkubwa jinsi wanavyoweza kutumia teknolojia ya kisasa katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre) inayotumika kuboresha huduma.



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (pichani), amewataka Wahandisi Wanawake wa Shirika hilo, kutembelea mashuleni ili kuwahamasisha (Motivate), wanafunzi wa kike ili wapende kujisomea masomo ya sayansi na Hisabati na hatimaye baadaye waje kushika nafasi kama walizo nazo wao.

Dkt. Mwinuka ameyasema hayo makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, wakati akiwapongeza Wahandisi wanawake wa Shirika hilo, baada ya kupewa tuzo na Makamu nwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuibuka wakwanza kwenye Kongamano la Wahandisi wanawake Tanzania “Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition, (TAWECE), ambalo huenda sambamba na maonesho ya shughuli za kihandisi lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

“Niwapongeze sana kwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye maonesho hayo, lakini niwaase, mpatapo nafasi mtembelee mashuleni ili muwahamasishe wanafunzi wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na hisabati, na kwa kupitia kwenu, wanaweza kujitokeza wasichana wengi kupenda masomo hayo na hivyo baadaye kufanya kazi za kihandisi kama nyinyi.” Alisema Dkt. Mwinuka.


Friday, August 25, 2017

MAMBO 6 MAZITO WALIYOIBUA LHRC LEO, SAKATA LA LISSU, BOMOA BOMOA, WAKEMEA MAUAJI

Katika kuisimamia na kulinda haki za binadamu nchini Tanzania Kituo cha sheria na hakiza binadamu Tanzania LHRC, Leo wameibuka na kukemea mambo kadhaa yanayoendelea nchini kwa sasa huku wakiitaka serikali kuyafanyia kazi kwa haraka kwani kuyaacha ni kuendelea kuminya haki za binadamu nchini,

Nchini Tanzania kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa kukiripotiwa mambo kadhaa ikiwemo Bomoa bomoa ya maeneo mbalimbali nchini kupisha shughuli za maendeeo,kamata kamata ya wanasiasa na kuminywa na democrasia nchini.Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na -------

SAKATA LA TANAPA KUJERUHI WANANCHI

Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam Kaimu mkurugenzi wa Kituo hicho Anna Henga ameyataja mambo ambayo wameamua kuishinikiza serikali kuyaangalia kwa jicho la Tati kuwa ni pamoja na Operation inayoendeshwa na TANAPA kulinda hifadhi ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakijeruhiwa na askari wa eneo hilo akiwemo kijana mmoja ambaye wamemtaka kwa jina la Pormoson Losso mwenye umri wa miaka 23 ambaye iliripotiwa kuwa alijeruhiwa kwa risasi na askari wa TANAPA kwa madai ya kuwa eneo la hifadhi,ambapo LHRC wamelitaka shirika hilo kuhakikisha kuwa linalinda haki za binadamu wakati likiendesha mazoezi yake kwani kutokufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi.

BOMOA BOMOA KIMARA

Sakata lingine ambalo LHRC wamelijadili ni kuhusu Bomoa bomoa inayoendelea ikiendeshwa na TANROADS katika barabara ya morogoro kupisha upanuzi wa barabara ambapo inasadikika kuwa mpaka sasa wakazi zaidi ya elfu moja wamebaki bila makazi maalum,huku wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto ambao wamaweza kupata madhara makubwa kwa hatua hiyo.


JAMBO LINGINE LITAKALO KUWEPO KWENYE TAMASHA LA JINSIA MWAKA HUU


TGNP Mtandao katika kutambua nafasi ya wanajamii imetoa nafasi maalum kwa watu waliofanya mambo makubwa kwenye jamii yao na mchango wao haukutambulika, hivyo watapewa nafasi ya kuadithia simulizi zao mpaka kufikia mafanikio aliyoyapata.

Hayo yalizungumzwa jana kwenye semina ya jinsia na maendeleo (GDSS) ilifanyika mapema kwenye ukumbi wa mtandao huo Mabibo jijini Dar es salaam.

Akiongoza semina hiyo afisa programu wa TGNP Mtandao Bw. Deogratius Temba alisema kuwa lengo kuu la tamasha hilo ni kusherekea mafanikio na kuangalia changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye harakati zao.

Amesema kuwa Wametoa nafasi hiyo kwa wanajamii na washiriki wa semina za jinsia na maendeleo kuwapa nafasi ya kusimulia stori za maisha yao kwa wale waliopitia magumu mpaka kufanikiwa na kutoa zawadi kwa waliofanya vizuri katika harakati za jinsia na maendeleo.

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA V 2017 AWAMU YA PILI


TAARIFA KWA UMMA

Ofisi ya Rais – TAMISEMI inapenda kuwajulisha wananchi juu Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano kwa Awamu ya Pili kwa mwaka 2017. Wanafunzi hawa wataanza muhula wa kwanza wa masomo tarehe 24 Agosti, 2017 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule.
Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 08 Septemba 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, atakuwa amepoteza nafasi.

Mwanafunzi mara uonapo jina lako kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwamba umechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, inabidi ku-download fomu ya kujiunga na shule husika kwenye mtandao.

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi awamu ya pili mwaka mwaka 2017 pamoja na fomu za kujiunga na shule (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz


MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MZEE WASIRA

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Stephen Wasira leo ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA


Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la chanzo cha mradi huu wa maji katika mji mdogo waIlula

Mkuu wa mkoa wa iringa Amina masenza akifurahia kufika kwenye chanzo cha maji pamoja na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kwa kuwa wanajua hilo ndio litakuwa suluhisho la mda mrefu kwa wakazi wa mji mdogo wa Ilula.


Na Fredy Mgunda,Iringa

Halmashauri ya wilaya ya kilolo inatarajia kutatua kero ya maji iliyodumu kwa miaka mingi katika mji mdogo wa Ilula mkoani Iringa kwa kutenga kiasi cha dola za kimarekani 9,548,827 kwa ajili ya kujenga chanzo kipya cha maji yatakayo weza kutatua changamoto hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekeleza wa ilani ya chama cha mapinduzi wilayani kilolo mkuu wa mkoa wa iringa ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya siasa ya mkoa bi Amina Masenza alisema kuwa wameamua kutafuta chanzo kipya ili kutatua tatizo la maji katika mji mdogo wa Ilula.

“Leo nimefika hadi huku kwenye chanzo cha maji ambacho naamini kuwa kitafanikiwa kutatua kero ya muda mrefu kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula hivyo lazima waisimamie ipasavyo ilani ya chama na kuhakikisha kuwa wanatatua matatizo ya wananchi”alisema Masenza


ZAIDI YA SH BILIONI 200 KUWANUFAISHA VIJANA NCHINI


PICHANI:Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(wa pili kushoto) akiwasili katika taasisi ya Chuo cha Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(NM-AIST) kuzindua mradi wa Vituo vya umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pamoja na mradi wa kuongeza ujuzi kwa kazi za uzalishaji zinazoleta tija uliofadhiliwa na Benki ya Dunia,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NM-AIST,Profesa David Mwakyusa na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo,Profesa Karoli Njau .

Filbert Rweyemamu,Arusha

Benki ya Dunia imetoa Sh 200 Milioni ili kuwezesha miradi ya elimu na ujuzi kwa ajili ya kazi zinazoleta uzalishaji wenye tija pamoja na vituo viwili vya umahiri vya kikanda vitakavyofungua ajira kwa vijana mara baada ya kuhitimu elimu.

Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo,Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa miradi hiyo itasaidia kuongeza watu wenye ujuzi wa kati ambao watafanya kazi katika sekta za kilimo,utalii,ujenzi ,nishati na madini.



RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU KAMISHNA MKUU WA TAKUKURU IKULU


Brigedia Jenerali John Julius Mbungo aliyeapishwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo

Thursday, August 24, 2017

KINANA AKUTANA NA MABALOZI WA NCHI 5 ZA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akiwa katika mazungumzo na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, alipokutana nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), akiwa na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, baada ya mazungumzo nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini.

PICHA: BASHIR NKOROMO. KWA PICHA ZAIDI ZA KIKAO HICHO ;BOFYA HAPA

SBL YATOA MAGARI MAWILI YA SHILINGI MILIONI 100

PICHANI: Meneja Masoko Mkoa wa Mwanza wa kampuni ya bia ya Serengeti Patrick Kisaka(kushoto) akimkabidhi funguo za gari mshindi wa usambazaji bora wa vinywaji vya kampuni hiyi Mkurugenzi wa kampuni ya Gramba Stanslaus Mmbaga, wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana.

Mwanza, Agosti 23 2017

Makampuni mawili ya usambazaji vinywaji jijini Mwanza kila moja yatunukiwa gari kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) kwa kuibuka wasambazaji wa juu wa bidhaa zake katika mikoa ya kanda ya ziwa. Makampuni hayo mawili - Gramba Limited kutoka wilaya ya Ilemela na Victoria General Supply Limited kutoka wilaya ya Nyamagana yote yakiwa yamejikita jijini Mwanza

Akikabidhi rasmi magari hayo kwenye sherehe iliyofanyika kiwandani hapo jijini Mwanza, Meneja wa kibiashara wa kikanda, Bwana Patrick Kisaka aliwapongeza washindi hao wawili kwa kujitolea kwao na kujituma kulikowapelekea kushinda gari hizo aina ya Eicher zenye thamani ya Shilingi 100m/=

Akitolea ufafanuzi, Kisaka alielezea kuwa Kampuni ya Gramba iliibuka mshindi kwenye kipengele cha uuzwaji wa pombe kali huku Kampuni ya Victoria General Supply ikiibuka mshindi kwenye kipengele cha msingi wa uuzwaji bidhaa.


Wednesday, August 23, 2017

MSHINDI WA MZUKA JACKPOT AKABIDHIWA MILIONI 80 DAR ES SALAAM LEO


PICHANI: Balozi wa Mchezo wa Bahati Nasibu wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya thamani ya shilingi milioni 80 Mshimdi Mkuu wa Mchezo huo, Rashid Ally katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Regence Mikocheni Jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mwakilishi kutoka Baraza la Michezo ya Bahati Nasibu Tanzania, Abdallah Hemed.

Na Dotto Mwaibale

MSHINDI Mkuu wa mchezo wa bahati nasibu ya Tatu Mzuka , Rashid Ally, leo amekabidhiwa sh.milinoni 80 alizojishindia katika droo kubwa iliyochezwa Jumapili.

Rashid ambaye alijishindia kiasi hicho cha fedha katika mchezo huo wa Tatu Mzuka, alionyesha kutoamini, huku akiwa na furaha na shukrani baada ya ushindi huo wa kihistoria. Rashid, ambaye ana umri wa miaka 21 tu, anaishi na familia yake maeneo ya Temeke, Dar es Salaam.

Akizungumzia ushindi wake, Rashid ambaye amemaliza kidato cha nne hivi karibuni, alisema kuwa alikuwa anacheza angalau mara 4 hadi 6 kwa wiki kwa kutumia pesa aliyokuwa anaipata katika shughuli zake za kila siku.

'Ndoto yangu ni kujenga nyumba, na kuwekeza katika kilimo, kitu ambacho nitafanya kwa kushirikiana na mama pamoja na Baba yangu. Nia yangu ni kuikuza iwe ni biashara kubwa ' alisema Rashid.


Tuesday, August 22, 2017

ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR Dk. SHEIN WILAYA YA MAGHARIBI "B"


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili katika ufunguzi wa jengo la madarasa 3 mapya katika Skuli ya Kijitoupele yaliyojengwa kwa nguvu za Wananchi kupitia Kampeni ya "MIMI NA WEWE" wakati wa ziara yake ya kutembelea maendeleo ya Miradi ya maendeleo Wilaya ya Magharibi"B" katika Mkoa wa Mjini Magharibi leo


Baadhi ya Wananchi na Wazee wa Wanafunzi katika Skuli ya Skuli ya Kijitoupele wakimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein mara alipowasili katika ufunguzi wa jengo la madarasa 3 mapya yaliyojengwa kwa nguvu za Wananchi kupitia Kampeni ya "MIMI NA WEWE" wakati wa ziara ya kutembelea maendeleo ya Miradi ya maendeleo Wilaya ya Magharibi"B" katika Mkoa wa Mjini Magharibi leo


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwapungia mkono Viongozi mbali mbali na Wananchi mara alipowasili katika ufunguzi wa jengo la madarasa 3 mapya ya Skuli ya Kijitoupele yaliyojengwa kwa nguvu za Wananchi kupitia Kampeni ya "MIMI NA WEWE" katika ziara yake ya kutembelea maendeleo ya Miradi ya maendeleo Wilaya ya Magharibi"B" katika Mkoa wa Mjini Magharibi

RIDHIWANI KIKWETE AKABIDHI ZAWADI ZA WACHEZAJI BORA NDONDO CUP

 Mbunge wa Chalinze Ridhiwani  Kikwete akizungumza na familia ya Wanamichezo wakati wautoaji wa Tunzo za Mchezaji borawa michuano ya Ndondo Cup inayoandaliw ana kampuni ya CloudsMedia Group kupitia kipindi chake cha Sports Extra
  Mbunge wa Chalinze Ridhiwani  Kikwete, akikabidhi tunzo ya Mchezaji bora kwa kocha wa timu ya Misosi FcYenye maskani  yake Manzese


DKT. KALEMANI AITAKA TANESCO KUUNGANISHA NGUVU KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME YA KURASINI NA KIMBIJI


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani,(pichani anayeongea), amelitaka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanakamilisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusamabaza umeme kinachotarajiwa kujengwa huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kalemani ametoa maelekezo hayo leo Agosti 22, 2017, wakati alipofanya ziara kukagua miradi ya umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini, Kigamboni na eneo panapotarajiwa kujengwa kituo kingine cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.

“Hakikisheni mradi wa uejenzi wa kituo hiki cha Kimbiji unakamilika ifikapo Machi 30, mwakani,(2018), na kuwaondolea adha ya upatikanaji wa umeme wananchi wa Kigamboni, chukueni mafundi waliokamilisha kazi ya kujenga kituo cha umeme kule Mtwara waje hapa, muwaache wale wanaojenga transition (njia ya kusafirisha umeme) wajenge, lakini wale mafundi wengine waleteni hapa ili mradi huu ukamilike.” Alifafanua.

Akiwa kwenye kituo cha kupoza na kusamabza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, Dkt. Kalemani aliipongeza TANESCO kwa juhudi kubwa walizofanya kwa hatua ujenzi waliyofikia ambapo sasa wameanza kufunga mashine kubwa. Kituo cha Kurasini ndicho kinachotegemewa sana na watu wa Mbagala, Kurasini na Kigamboni.

Monday, August 21, 2017

UBER YAZINDUA HUDUMA YA MADEREVA NA WASAFIRI KUCHATI KWA KUTUMIA PROGRAMU HIYO


Dar es Salaam Tarehe 21 Agosti 2017…Kampuni ya Uber nchini Tanzania imetangaza zana mpya maarufu kama “Kuchati Ndani ya Programu” inayowawezesha madereva na wasafiri kuandikiana ujumbe kwa kutumia programu hiyo bila malipo.

Kinyume na hapo awali ambapo madereva na wasafiri wangetumia Ujumbe Mfupi (SMS) au kupiga simu, zana hii inaleta unafuu kwa madereva na wasafiri hivyo basi kuwapunguzia kadhia ya gharama za kupiga simu sambamba na kuharakisha mawasiliano bila kuondoka kwenye programu ya Uber.

Maboresho haya ni juhudi endelevu za Uber na yanalenga kuimarisha wigo wa wasafiri na madereva wanapotumia programu ya Uber.

Zana hii mpya ni rahisi sana kuitumia. Msafiri anapoita gari, kuna kitufe cha ‘Kuwasiliana’ kwenye menyu inayoonekana chini ya skrini. Wasafiri wanaweza kuwaandikia ujumbe madereva, na madereva vivyo hivyo. Ujumbe utaonesha kwamba umepokelewa baada ya kuutuma.

Kwa upande mwingine, madereva watakiri kwamba wamesoma ujumbe kwa kugusa kwenye programu ya Uber ili watume ujumbe wa ‘bomba’. Ili wasijichanganye barabarani. Aidha wasafiri na madereva wanaweza kuona kama ujumbe wao waliotuma umesomwa.

Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania Bw. Alfred Msemo amehoji kwamba, “Kila safari nzuri huanza pale msafiri anapochukuliwa kwa gari, kwa hiyo tunajituma kutafuta mbinu za kumchukua msafiri bila usumbufu wowote kwa msafiri au dereva. Kipengele hiki cha Kuchati kitakuwa afueni kwa wasafiri na madereva wanapotaka kuwasiliana ili kusaidiana kutafuta mwafaka wa changamoto za safari kama vile, kufungwa kwa barabara au kutoa maelezo ya mahali walipo.”