Monday, June 12, 2017

SOMA RIPOTI YA PILI ILIYOCHUNGUZA MAKINIKIA ILIYOWASILISHWA LEO MBELE YA RAIS MAGUFULI

MUHTASARI WA RIPOTI YA KAMATI MAALUM YA KUCHUNGUZA MASUALA YA KISHERIA NA KIUCHUMI KUHUSIANA NA MCHANGA WA MADINI UNAOSAFIRISHWA NJE YA NCHI
Utangulizi
Mheshimiwa Rais,
Kama ambavyo Watanzania watakumbuka tarehe 10 Aprili 2017, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliteua Kamati Maalum ya Kuchunguza Masuala ya Kisheria na Kiuchumi Kuhusiana na Mchanga wenye Madini unaosafirishwa nje ya nchi yakiwemo makontena 277 yaliyozuiliwa na Serikali katika Bandari ya Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ni:
  1. Prof. Nehemiah Eliakim Osoro (Mwenyekiti)
  2. Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara
  3. Dr. Oswald Joseph Mashindano
4 Bw. Gabriel Pascal Malata
  1. Bw. Casmir Sumba Kyuki
  2. Bi. Butamo Kasuka Philip
  3. Bw. Usaje Benard Asubisye
  4. Bw. Andrew Wilson Massawe
1
Mheshimiwa Rais,
katika kutekeleza uchunguzi huo, Kamati Maalum iliongozwa na Hadidu za Rejea zifuatazo:

  1. Kufanya tathmini ya mchakato mzima wa usafirishaji wa makinikia na kujiridhisha iwapo utaratibu huo unafanyika kwa mujibu wa Mikataba iliyoingiwa baina ya Serikali na Makampuni ya uchimbaji wa madini “Mining Development Agreements” (MDAs) na “Special Mining Licence” (SPL) na kwamba taratibu hizo zinafuatwa kikamilifu. Pamoja na masuala mengine ambayo Kamati itaona ni muhimu kuyafuatilia, Kamati ijiridhishe kuhusu mrejesho wa taarifa za uchenjuaji wa makinikia kutoka nje ya nchi kwa mamlaka za Serikali.
  2. Kupitia Mikataba husika na kushauri endapo inazingatia kikamilifu maslahi ya nchi ama inahitaji kuboreshwa. Maeneo yenye mapungufu na mapendekezo ya maboresho yabainishwe wazi.
  3. Kufanya tathmini ya mfumo mzima wa udhibiti kuhusu biashara ya makinikia kutoka kuchimbwa, kusafirishwa, kuyeyushwa na kuuzwa kwa madini yanayopatikana katika makinikia hayo kwa lengo la kubainisha ufanisi wa mfumo huo katika kuzuia upotevu wa mapato ya
2
Serikali yanayotokana na usafirishaji wa makinikia nje ya nchi.
  1. Kupitia taarifa ya Kamati ya Wataalam ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyomo kwenye makontena yenye makinikia ya dhahabu yaliyokusudiwa kusafirishwa nje ya nchi, iliyoteuliwa tarehe 29 Machi 2017, hususan, kuhusu aina, kiasi, viwango vya ubora na thamani za madini yaliyomo kwenye makinikia hayo na kubainisha kama Serikali inapata mapato stahiki ya kikodi kutokana na biashara hiyo kwa mujibu wa mikataba na sheria za nchi.
  2. Kubaini idadi ya makontena yenye makinikia yaliyosafirishwa kutoka katika migodi ya dhahabu kuanzia mwaka 1998 hadi sasa; na kwa kuzingatia taarifa ya Kamati ya Wataalam iliyotajwa katika aya ya 4, Kamati ifanye makadirio ya kiasi cha mapato ambacho Serikali ingestahili kupata na kulinganisha na kiasi halisi cha mapato kilichopatikana katika kipindi hicho.
  3. Kubaini na kujiridhisha kama kuna sababu zozote za msingi za kiuchumi na kiufundi zinazokwamisha uanzishwaji wa kiwanda cha kuyeyusha makinikia

3
nchini na kuishauri Serikali ipasavyo. Taarifa hiyo ibainishe:
  1. Nini kinahitajika ili teknolojia ya kuchenjua mchanga kuwepo hapa nchini;
  2. Ni gharama kiasi gani zinahitajika ili kuanza uchenjuaji wa makininkia hapa nchini;
  3. Inachukua muda gani kukamilisha ujenzi wa mtambo husika hadi kuanza kufanya kazi;
  4. Nchi ina uwezo au mapungufu gani katika
    kulitekeleza hilo hasa katika upande wa
    wataalam na uwekezaji.
(v) Aidha, Kamati ibainishe na kujiridhisha kuhusu
hatua zilizochukuliwa na kampuni za uchimbaji dhahabu nchini katika kutekeleza sera na sheria za nchi kuhusu uanzishwaji wa kiwanda cha kuchenjua makinikia.
7. Kuchunguza na kulinganisha taarifa za uchunguzi wa kimaabara wa makinikia zinazotolewa na kampuni ya SGS Tanzania Superintendence Company LTD (maabara binafsi inayopima sampuli za makinikia ya kampuni za madini) na Wakala wa Uchungzi wa Madini Tanzania (Tanzania Mineral Audit Agency –TMAA). Aidha, Kamati ibainishe ushiriki na majukumu ya kampuni nyingine ikiwamo SGS kuhusu makinikia.
4
8. Kubainisha uwepo wa mikataba na maudhui yake kati ya kampuni za uchimbaji madini ya dhahabu Tanzania na kampuni za uchenjuaji wa makinikia yanoyosafirishwa ili kijiridhisha kuhusu uhalali wa biashara hiyo na kama kodi na tozo mbalimbali za Serikali zililipwa ipasavyo.
  1. Kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na mchakato mzima wa usafirishaji wa makinikia, na kutoa mapendekezo ya kuboresha taratibu husika kwa siku zijazo kwa maslahi ya nchi.
  2. Kufanya kazi kwa karibu na wataalamu katika Sekta ya Madini waliobobea katika taaluma zao wakiwemo Wanajiolojia, Wahandisi wa uchenjuaji (Metallurgists), Wakemia (Chemists), Wataalamu wa masuala ya Fedha na Wachumi pamoja na wataalam wa masuala ya sheria na kodi, kadri itakavyoona inahitajika.
  3. Endapo itafaa, kuongeza Hadidu za Rejea katika kuboresha utekelezaji wa majukumu yake. Aidha, Kamati itakuwa na mamlaka ya kumwita mtu yeyote au kuwasiliana na ofisi yoyote ya Serikali (kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi) kwa lengo la kupata taarifa muhimu zinazohitajika.
5
Utekelezaji wa Majukumu Mheshimiwa Rais,
Katika kutekeleza uchunguzi huo, Kamati ilifanya mambo yafuatayo:
  1. Kuandaa Mpango Kazi, kukusanya na kupitia mikataba, sheria, sera za madini na kodi, hususan mikataba ya utafiti, uchimbaji, usafirishaji na uuzaji wa madini na makinikia, kuchambua na kuhakiki mfumo mzima wa udhibiti wa biashara ya makinikia, na taarifa kupokea taarifa kutoka mamlaka za Serikali nchini na nje ya nchini kuhusiana na uchenjuaji wa makinikia.
  2. Kutembelea na kupata taarifa kutoka sehemu na taasisi zifuatazo:
    1. Migodi ya Bulyanhulu Gold Mines Ltd (Acacia Gold Mining Plc), Pangea Gold Mine Ltd (Acacia Gold Mining Plc), North Mara Gold Mine Ltd (Acacia Gold Mining Plc), Geita Gold Mine Ltd (AngloGold Ashanti Ltd);
    2. Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa lengo la kuona na kupima uzito wa makontena 277 yenye makinikia yaliyozuiliwa na Serikali; na
    3. Mamlaka ya Mapato Tanzania, Ofisi Kuu ya Takwimu, Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa
6
Ukaguzi wa Madini Tanzania(TMAA), Shirika la Madini Tanzania(STAMICO) na Ofisi ya Msajili wa Makampuni (BRELA), Mamlaka ya Masoko ya Hisa na Mitaji (CMSA);
3. Kuwaita na kufanya mahojiano na:
i. Watendaji wakuu Serikalini na watumishi wa

taasisi za Serikali na binafsi; na
ii. Watu binafsi wenye ujuzi na uzoefu katika sekta ya

madini, usafirishaji wa mizigo na wakala wa meli.
  1. Kupata taarifa na kujifunza kutoka kwenye nchi nyingine zilizofanikiwa katika biashara ya madini na uchenjuaji wa makinikia.
  2. Kukusanya na kufanya uchambuzi wa takwimu za makontena ya makinikia yaliyosafirishwa nje ya nchi na takwimu za kiuchumi na kodi ili kubaini kodi halisi iliyolipwa na kodi ambayo ilipaswa kukusanywa kutokana na biashara ya uuzaji wa makininkia nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2017.
  3. Kufanya uchambuzi kuhusu uwezekano wa ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji wa makinikia nchini.
  4. Kufanya uchambuzi wa taarifa za kimaabara za makinikia zilizotolewa na kampuni ya maabara binafsi inayopima sampuli za makinikia ya madini (SGS),
7
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na Kamati Maalum Namba 1.
Matokeo ya Uchunguzi
Mheshimiwa Rais
1. Uhalali wa Kisheria wa Kampuni ya Acacia Mining Plc nchini Tanzania.
Kamati imebaini na kuthibitisha kwa mujibu wa nyaraka na maelezo kutoka ofisi ya Msajili wa Makampuni (BRELA) kuwa kampuniya Acacia Mining Plc haikusajiliwa (incorporation) nchini Tanzania na wala haina hati ya utambuzi (certificate of compliance) kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni, Sura ya 212.
Kamati pia imebaini kuwa kampuni ya Acacia Mining Plc, ambayo inajinasibisha kuwa mmiliki wa makampuni ya Bulyanhulu Gold Mines Ltd, North Mara Gold Mine Ltd na Pangea Minerals Ltd, haikuwahi kuwasilisha nyaraka wala taarifa yoyote kuonesha kuwa kampuni hiyo ni mmiliki wa makampuni hayo wala kuwa na hisa katika makampuni hayo. Kwa kuwa Acacia Mining Plc haina usajili wala utambuzi wa kisheria nchini Tanzania, haina sifa ya kupata
8
leseni, kuchimba wala kufanya biashara ya madini nchini Tanzania.
Hivyo basi, Kamati imebaini kuwa Acacia Mining Plc, inafanya biashara ya madini hapa nchini kinyume cha sheria za nchi.
2. Biashara ya Uuzaji na Usafirishaji wa Makinikia Nje ya Nchi
Mheshimiwa Rais,
Kamati ilibaini kuwa makampuni ya Bulyanhulu Gold Mines Ltd na Pangea Minerals Ltd ndizo wazalishaji na wauzaji wa makinikia nje ya nchi. Kwa mujibu wa mikataba ya mauzo ya makinikia baina ya makampuni hayo na wafanyabiashara kutoka nje ya nchi, makinikia husafirishwa kutoka Tanzania yakiwa yameshauzwa na hupelekwa nje ya nchi kwa madai ya kwenda kuchenjuliwa kupitia Bandari za Dar es Salaam na Tanga. Makinikia hayo hupelekwa nchi za China, Japani na Ujerumani, yakiwa kwenye makontena yenye urefu wa futi 20 na wastani wa tani 20 kila moja. Wafanya biashara wa makinikia ni makampuni yaitwayo Aurubis AG na Aurubis Bulgaria ADM, Mark Rich Co. Investment AG na Pan Pacific Copper Co. Limited kutoka nchi za Ujerumani, Uswisi na Australia. Mauzo hayo ya makininkia hufanywa kwa mujibu wa mikataba ya uchimbaji wa madini kati ya Serikali na Makampuni ya uchimbaji madini (Mining Development
9
Agreements-MDAs). Kutokana na taarifa za kiuchunguzi (forensic investigation) kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mauzo ya makininkia hufanyika kupitia Ofisi ya Uhasibu (Treasury Department) ya makampuni hayo iliyopo Afrika ya Kusini.
3. Utaratibu wa Uuzaji Makinikia Nje ya Nchi
Mheshimiwa Rais,
Kamati imebaini kwamba kifungu cha 51 cha Sheria ya Madini kinaruhusu mwenye leseni ya uchimbaji wa madini kufanya biashara ya madini, ikiwa ni pamoja na kuuza nje ya nchi. Kifungu hicho kinamtaka mwenye leseni ya uchimbaji kupata kibali cha kusafirisha madini kutoka kwa Afisa Mwenye Mamlaka atayethibitisha kwamba mrahaba stahiki umelipwa kwa Serikali. Mbali ya kupata kibali kinachoonesha malipo ya mrahaba hakuna utaratibu mwingine maalum katika biashara ya uuzaji na usafirishaji wa makinikia nje ya nchi. Aidha, kisheria makampuni ya madini yanapaswa kutoa taarifa sahihi kwa Serikali kuhusu aina, kiasi na thamani ya madini yaliyomo ili kuiwezesha Serikali kukokotoa na kutoza mrahaba stahiki.
Mheshimiwa Rais,
Kwa kuzingatia nyaraka na taarifa mbalimbali za kiuchunguzi, Kamati imeridhika kuwa baadhi ya watumishi wa Serikali, watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini,
10
makampuni ya usafirishaji na upimaji wa madini na makampuni yenyewe yametenda makosa mbalimbali ya kijinai yakiwemo ukwepaji wa kodi, kutoa taarifa za uwongo, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu, uhujumu uchumi na kulisababishia taifa hasara kinyume cha:
  1. vifungu vya 18,114 na 115 vya Sheria ya Madini, 2010
  2. vifungu vya 101 na 106 vya sheria ya kodi ya mapato, 2004
  3. vifungu vya 79 na 82 vya Sheria Usimamizi wa kodi, 2015
  4. kifungu cha 24 cha Sheria ya Uwazi na uwajibikaji katika sekta ya Madini Tanzania, 2015
  5. Kifungu cha 27 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi sura ya 200, na
  6. Kifungu cha 203 cha Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,2004
Kwa kuzingatia nyaraka na taarifa mbali mbali za kiuchunguzi Kamati pia imeridhika kuwa baadhi ya watumishi wa Serikali, watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini, makampuni ya usafirishaji na upimaji wa madini na makampuni yenyewe wamelitia aibu Taifa kwa kutenda makosa mbali mbali yakiwemo, ukwepaji wa kodi, kutoa taarifa za uwongo, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu, uhujumu uchumi na kulisababishia taifa hasara.
11
Mheshimiwa Rais,
Kamati pia imebaini kwamba, katika kufanya biashara ya makinikia makampuni ya Bulyanhulu na Pangea yamekuwa yakiuza makinikia nje ya nchi pasipo kufuata utaratibu kwa namna ambayo vitendo vifuatavyo vimedhihirika:
i. Udanyanyifu wa kibiashara na ukwepaji wa kodi ambao umesababisha:
  1. Kuficha idadi, uzito na thamani ya madini yaliyomo kwenye makontena 277 yaliyozuiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa kiwango cha wastani kuonesha kwamba thamani yake ni TZS 79,939,900,989.49 (TZS 79.94 bilioni), wakati thamani halisi, kwa mujibu wa uchunguzi wa kimaabara uliofanywa na Kamati Maalum Na. I, unaonesha kuwa thamani halisi ya madini yaliyomo, ni kati ya TZS 829,361,455,861 (TZS 829.36 bilioni) kwa kiwango cha chini, na TZS 1,438,760,551,512 (TZS 1.438 trilioni) kwa kiwango cha juu.
  2. Mgongano au kusigana kwa taarifa za uzito na idadi ya makontena kati ya nyaraka za kusafirishia makontena (kadhia) ukilinganisha na nyaraka za wakala wa meli (shipping orders). Idadi na uzito wa makontena ikiwa kubwa zaidi kwenye nyaraka za wakala wa meli kuliko kadhia (export entry) zilizotengenezwa na makampuni hayo kwa lengo la kusafirishia makontena nje ya nchi.
12
c. Kiasi cha mrahaba kilichooneshwa katika vitabu vya hesabu za makampuni ya Bulyanhulu na Pangea zimeonesha kwamba, Dola za Marekani 111,304,561.00 (USD 111.3 milioni) zililipwa Serikalini kama mrahaba kati ya mwaka 1998 na 2017, lakini vitabu vya hesabu vilivyopo Wizara ya Nishati na Madini zinaonesha malipo yalikuwa Dola za Marekani 42,702,727.50 (USD 42.7 milioni). Hali hii inaonesha upungufu wa kiasi cha Dola za Marekani 68,601,833.50 (USD 68.6 milioni) zilizopaswa kulipwa kama mrahaba.
  1. Makampuni ya wakala wa meli ya Freight Forwarders (T) Limited, Quick Services Clearing and Forwarding Limited na Walford Meadows Co. Ltd, ziliwasilisha nyaraka za uwongo za usafirishaji wa makinikia kutoka Kahama Mining Corporation, (baadaye Bulyanhulu Gold Mine Ltd) na Pangea Minerals Ltd, katika kipindi cha kati ya mwaka 1998 na 2017.
  2. Kutoa taarifa za uwongo za uchenjuaji nje ya nchi wakati makanikia hayo yameuzwa kabla ya kusafirishwa kutoka Tanzania kupelekwa nchi za nje.
ii. Kufanya magendo katika biashara ya makinikia:
a. Makontena 30 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia yameelezwa kwenye hati ya usafirishaji nje ya nchi Na.1482 ya tarehe 23.7.2001. Hata hivyo,
13
iligundulika kupitia hati ya usafirishaji melini Na. TZGT00000552 kuwa makontena 33 yenye urefu wa futi 20 ndiyo yalisafirishwa na kwa sababu hiyo yakionyesha makontena matatu zaidi ya idadi iliyooneshwa kwenye hati ya usafirishaji melini iliyoandaliwa na wakala wa usafirirshaji, kwa niaba ya makampuni ya uchimbaji madini.
  1. Makontena 60 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia yameelezwa kwenye hati ya usafirishaji nje ya nchi Na. 1483 ya tarehe 7.8.2001. Hata hivyo, iligundulika kupitia hati ya usafirishaji melini Na. MOL-1 ya makontena hayo hayo, kuwa makontena 67 yenye urefu wa futi 20 ndiyo yalisafirishwa na kwa sababu hiyo, ikiwa ni makontena saba (7) zaidi ya idadi iliyooneshwa na wakala wa usafirishaji, kwa niaba ya makampuni ya uchimbaji madini.
  2. Makontena 48 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia yameelezwa kwenye hati ya usafirishaji nje ya nchi Na.1487 ya tarehe 27.8.2001. Hata hivyo, iligundulika kupitia hati ya usafirishaji melini Na. Mol-100038 kuwa makontena 67 yenye urefu wa futi 20 yalisafirishwa na kwa sababu hiyo yakionyesha makontena kumi na tisa (19) zaidi ya idadi iliyooneshwa kwenye hati ya usafirishaji melini iliyoandaliwa na wakala wa usafirirshaji kwa niaba ya makampuni ya uchimbaji madini.
14
d. Makontena 85 ya urefu wa futi 20 yenye makinikia yameelezwa kwenye hati ya usafirishaji nje ya nchi Na.1504 ya tarehe 20.12.2001. Hata hivyo, iligundulika kupitia hati ya usafirishaji melini Na. Mol-01 kuwa makontena 99 yenye urefu wa futi 20 ndiyo yalisafirishwa na kwa sababu hiyo yakionesha makontena kumi na nne (14) zaidi ya idadi iliyooneshwa kwenye hati ya usafirishaji melini iliyoandaliwa na wakala wa usafirishaji, kwa niaba ya makampuni ya uchimbaji madini.
iii. Ukwepaji wa kodi ya mapato kwa njia ya udanganyifu wa bei ya bidhaa au huduma (transfer price manipulation).
  1. Mauzo ya makinikia kwa wafanyabiashara na wachenjuaji nje ya nchi hayakufanyika kwa ushindani kutokana na kuonesha vipindi virefu vya uhusiano wa kibiashara kwa kuzingatia nyaraka za mikataba baina yao.
  2. Masharti ya usafirishaji wa makinikia ulionyeshwa kuwa free on board (f.o.b) badala ya cost and freight (c.fr) au cost, insurance and freight (c.i.f) makanikia hayo yaliuzwa kwa wafanya biashara wale wale na wachenjuaji wale wale wenye
15
mahusiano ya kibiashara kama ilivyooneshwa katika mikataba ya mauzo ya makinikia baina yao.
c. Madini yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia hasa badala yake, yalikuwa ni madini ya aina mbali mbali mahususi yaliyopatikana kutokana na uchenjuaji kwa njia ya ‘carbon–in- leach’ (CIL).
  1. Upandishaji wa gharama za uendeshaji migodi:
    Uchunguzi wa kisayansi wa mifumo ya computa (forensic examination kupitia TRA, umebaini kwamba gharama za utafutaji na upembuzi wa miamba yenye madini imejumuishwa kwenye gharama za mauzo na kwa sababu hiyo, kuathiri faida halisi ambayo ilipaswa kutozwa kodi. Hali hii imesababisha faida ya makampuni kutoonekana na kwa sababu hiyo kuathiri msingi wa ukokotoaji kodi ya mapato ya makampuni (tax base for corporate tax).
  2. Mrahaba ambao haukukusanywa
    Kwa mujibu wa taarifa za mwaka 2007, 2011 na 2012 zilizotolewa na PriceWater Coopers, bei ya dhahabu katika soko la kimataifa imekuwa ikipanda na kuwezesha makampuni ya madini kupata faida zaidi ya asilimia 1,400 mwaka 2002 na 2006 ambapo
16
Bulyanhulu na Pangea, zilipata faida ya asilimia 32. Hata hivyo, faida yote iliyopatikana kutokana na kupanda kwa bei ya dhahabu haikuoneshwa kwa madhumuni ya malipo ya mrahaba kwa Serikali.
vi. Uhamishaji haramu wa fedha
Uchunguzi wa kisayansi na mifumo ya komputa kupitia TRA imebainika kuwa faida iliyooneshwa na Kampuni mama (Holding Company) iliyopo nje ya nchi ya Tanzania imekuwa ikirudishwa kwenye makampuni ya uchimbaji nchini kama mikopo iliyotolewa na riba zake. Baadaye riba inayotozwa kwenye taarifa za hesabu Kama gharama kwa makampuni ili kutumika katika kukokotoa kodi ya mapato ya kampuni (Assessment of Corporate Income Tax).
Thamani ya Madini Yalimo kwenye Makinikia Kwenye Makontena 44,277
Mheshimiwa Rais,
Uchunguzi wa Kamati ulibaini kuwepo takwimu mbali mbali za idadi ya makontena yaliyosafirishwa nje nchi kuanzia mwaka 1998 hadi mwezi Machi 2017. Hata hivyo, Kamati iliamua kutumia takwimu kutoka Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa (TRA) kwa kuwa, moja ya majukumu ya idara hiyo ni kukusanya takwimu za bidhaa zote zinazosafirishwa nje ya nchi kupitia bandari, viwanja vya ndege na mipaka
17
ya nchi. Kutokana na chanzo hicho idadi ya makontena yaliyosafirishwa yalikuwa 44,277 kwa kiwango cha chini na makontena 61,320 kwa kiwango cha juu kutoka kwenye vyanzo vyetu vya uchunguzi.
Viwango vya Dhahabu kwenye Makinikia
Mheshimiwa Rais,
Viwango vya dhahabu vilikuwa na wastani wa 28 kg za dhahabu kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha dhahabu kwenye kila kontena, makontena 44,277 yatakuwa na dhahabu kiasi cha tani 1,240. Kiasi hiki kina thamani ya TZS 108,062,091,984,000 (TZS 108.06 trilioni), sawa na USD 49,119,132,720 (USD 49.12 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha dhahabu kwa kontena moja (47.5 kg), kiasi cha dhahabu katika makontena 44,277 kitakuwa tani 2,103 ambazo thamani yake ni TZS 183,319,620,330,000 (TZS 183.32 trilioni), sawa na USD 83,327,100,150 (USD 83.32 bilioni).
Viwango vya Madini ya Silver, Copper, Sulphur, Iron, Nickel na Zinc kwenye Makinikia
Madini ya Silver
Kiwango cha Silver kilikuwa ni wastani wa 6.1 kg kwa kila kontena. Kwa kutumia kiwango hicho kwa kila kontena, makontena 44,277 yatakuwa na Silver kiasi cha tani 270. Kiasi hiki kina thamani ya TZS 329,660,684,232 (TZS 329.66 bilioni),
18
sawa na USD 149,845,766 (USD 149.8 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu katika kontena moja (7 kg) kiasi cha Silver katika makontena 44,277 kitakuwa tani 309 ambazo thamani yake ni TZS 378,299,145,840 (TZS 378.3 bilioni) sawa na USD 171,954,157 (USD 172 milioni).
Madini ya Copper
Kiwango cha copper kilikuwa na wastani wa 5,200 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha copper kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na copper kiasi cha tani 230,240. Kiasi hiki cha copper kina thamani ya TZS 2,861,888,172,000 (TZS 2.86 trilioni) sawa na USD 1,300,858,260 (USD 1.3 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha copper kwa kontena moja (6,756 kg), kiasi cha copper katika makontena 44,277 kitakuwa tani 299,135 ambazo thamani yake ni TZS 3,718,253,171,160 (TZS 3.72 trilioni) sawa na USD 1,690,115,078 (USD 1.692 bilioni)).
Madini ya Sulphur
Kiasi cha Sulphur kilikuwa na wastani wa 7,800 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha Sulphur kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na Sulphur kiasi cha tani 345,360. Kiasi hiki cha Sulphur kina thamani ya TZS 227,937,996,000 (USD 103,608,180). Kwa kutumia kiwango cha juu cha sulphur kwa kontena moja lenye uzito wa 10,160 kg, kiasi cha Sulphur katika makontena 44,277 kitakuwa tani 449,854 ambazo thamani yake ni TZS
19
296,903,851,200 (TZS 296.9 bilioni), sawa na USD 134,956,296 (USD134.96 milioni).
Madini ya Iron
Kiwango cha iron kilikuwa na wastani wa 5,400 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha iron kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na iron kiasi cha tani 239,095. Kiasi hiki cha iron kina thamani ya TZS 368,207,532,000 (USD 167,367,060). Kwa kutumia kiwango cha juu cha iron kwa kontena moja lenye uzito wa 6,100 kg, kiasi cha iron katika makontena 44,277 kitakuwa tani 270,089 ambazo thamani yakeni ni TZS 415,938,138,000 (TZS 415.94 bilioni), sawa na USD 189,062,790 (USD 189.06 milioni).
Madini ya Nickel na Zinc
Zinc
Kiwango cha zinc kilikuwa ni wastani wa 5,400 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha zinc kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na zinc kiasi cha tani 1,474. Kiasi hiki cha zinc kina thamani ya TZS 8,433,705,852 (TZS 8.43 bilioni) sawa na USD 3,833,503 (USD 3.83 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwa makontena moja (65.8 kg) kiasi cha zinc katika makontena 44,277 kitakuwa na uzito wa tani 2,913 kg ambazo thamani yake ni TZS 16,664,800,152 (TZS16.66 bilioni), sawa na USD 7,574,909 (USD 7.57 milioni).
20
Nickel
Kiwango cha nickel kilikuwa ni wastani wa 5,400 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha nickel kwenye kila makontena, makontena 44,277 yatakuwa na nickel kiasi cha tani 620. Kiasi hiki cha nickel kina thamani ya TZS 13,228,196,520 (6,012,817). Kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwa makontena moja kiasi cha inickel katika makontena 44,277 kitakuwa tani 1,771 ambazo thamani yakeni ni TZS 37,794,847,200 (USD 17,179,476).
Madini ya kundi la Platinum
Rhodium
Viwango vya rhodium vilikuwa na wastani wa 0.034 kg za rhodium kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha rhodium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na rhodium kiasi cha tani 1.5. Kiasi hiki cha rhodium kina thamani ya TZS 105,754,560,707 (TZS 105.75 bilioni), sawa na USD 6,012,817 (USD 6.01 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha rhodium kwa kontena moja 0.078 kg, kiasi cha rhodium katika makontena 44,277 kitakuwa tani 3.5 kg ambazo thamani yake ni TZS 242,613,403,976 (TZS 242.6 bilioni), sawa na USD 110,278,820 (USD 110.28 milioni).
21
Iridium
Kiwango cha iridium kilikuwa ni wastani wa 6.4 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha iridium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na iridium kiasi cha tani 283. Kiasi hiki cha iridium kina thamani ya TZS 17,187,693,811,200 (TZS 17.19 trilioni), sawa na USD 7,812,588,096 (USD1.8 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu iridium kwa makontena moja 13.75 kg, kiasi cha iridium katika makontena 44,277 kitakuwa tani 609 kg ambazo thamani yake ni TZS 36,926,685,922,500 (TZS 36.93 trilioni), sawa na USD 16,784,857,238 (USD 16.9 bilioni).
Viwango vya Metali za Rare Earth Elements (REE), Transition Elements na Light Elements
Ytterbium
Kiwango cha ytterbium kilikuwa ni wastani wa 3.7 kg za ytterbium kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha ytterbium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na ytterbium kiasi cha tani 164. Kiasi hiki cha ytterbium kina thamani ya TZS 1,982,281,290,000 (TZS 1.98 trilioni), sawa na USD 901,036,950 (USD 901 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu ytterbium kwa kontena moja 4.9 kg, kiasi cha ytterbium katika makontena 44,277 kitakuwa tani 217 kg ambazo thamani yake ni TZS 2,625,183,330,000 (TZS 2.63 trilioni), sawa na USD 1,193,265,150 (USD 1.2 bilion).
22
Beryllium
Kiwango cha beryllium kilikuwa wastani wa 19.4 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha beryllium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na beryllium kiasi cha tani 859. Kiasi hiki cha beryllium kina thamani ya TZS 956,209,634,160 (TZS 956.2 bilioni), sawa na USD 434,640,743 (USD 434.64 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha beyllium kwa kontena moja 26.9 kg kiasi cha beryllium katika makontena 44,277 kitakuwa tani 1,310 kg ambazo thamani yake ni TZS 1,325,878,307,160 (TZS1.32 trilioni), sawa na USD 602,671,958 (USD 602.67 milioni).
Tantalum
Kiwango cha tantalum kilikuwa ni wastani wa 11.7 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha tantalum kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na tantalum kiasi cha tani 518. Kiasi hiki cha tantalum kina thamani ya TZS 300,878,154,720 (TZS 300.87 bilioni), sawa na USD 136,762,798 (USD 136.76 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu kilichopimwa kwa kontena moja (17.3 kg), kiasi cha tantalum katika makontena 44,277 kitakuwa tani 766 kg ambazo thamani yake ni TZS 444,888,211,680 (TZS 444,88 bilioni), sawa na USD 202,221,914 (USD 202.2 milioni).
23
Lithium
Kiwango cha lithium kilikuwa wastani wa 21.5 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha lithium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 44,277 yatakuwa na lithium kiasi cha tani 952. Kiasi hiki cha lithium kina thamani ya TZS 164,821,575,270 (TZS 164.82 bilioni), sawa na USD 74,918,898 (USD 74.91 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu lithium kwa kila kontena moja lenye 29.8 kg, kiasi cha lithium katika makontena 44,277 kitakuwa tani 1,319 ambazo thamani yake ni TZS 228,450,369,444 (TZS 228.4 bilioni), sawa na USD 103,841,077 (USD 103.84).
Mheshimiwa Rais,
Jumla ya thamani ya madini katika makontena 44,077 yaliyosafirishwa nje ya nchi katika kipindi cha mwaka 1998 hadi 2017 kwa kutumia kiwanjumla ya thamani ya madini katika makontena 44,077 kwa kutumia kiwango cha wastani ni TZS 132,569,087,296,991 (TZS 132.56 trilioni) sawa na USD 60,258,676,044 (USD 60.25 bilioni) au TZS 229,977,173,828,312 (TZS 229.9 trilioni) sawa na USD 104,535,079,013 (USD 104.5 bilioni.) kwa kiwango cha juu.
24
Thamani ya Madini Yaliyomo kwenye Makinikia Kwenye Makontena 61,320
Viwango vya Dhahabu
Kiwango cha dhahabu kwenye makinikia kilikuwa ni wastani wa 28 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha dhahabu kwenye kila kontena la tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na dhahabu kiasi cha tani 1,717. Kiasi hiki cha dhahabu kina thamani ya TZS 149,657,101,440,000 (TZS 149.65 trilioni), au USD 68,025,955,200 (TZS 68 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha dhahabu kwa kontena moja kwa uzito wa 47.5 kg, kiasi cha dhahabu katika makontena 61,320 kitakuwa tani 2,913 ambazo thamani yake ni TZS 253,882,582,800,000 (TZS 253.8 trilioni), sawa na USD 115,401,174,000 (USD 115 bilioni).
Viwango vya Madini ya Silver, Copper, Sulphur, Iron, Nickel na Zinc kwenye Makinikia
Madini ya Silver
Kiwango cha Silver kilikuwa wastani wa 6.1 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha silver kwenye kila makontena la uzito wa tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na Silver kiasi cha tani 20. Kiasi hiki cha Silver kina thamani ya TZS 456,552,909,120 (TZS 456.55 bilioni) sawa na USD 207,524,050 (USD207.5 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha silver kwa kontena moja, 7 kg kiasi cha Silver katika
25
makontena 61,320 kitakuwa tani 429 ambazo thamani yake ni TZS 523,913,174,400 (TZS 523.9 bilioni), sawa na USD 238,142,352 (USD 238.1 milioni).
Madini ya Copper
Kiwango cha copper kilikuwa wastani wa 5,200 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha copper kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na copper kiasi cha tani 318,864. Kiasi hiki cha copper kina thamani ya TZS 3,963,479,520,000 (TZS 3.9 trilioni), sawa na USD 1,801,581,600 (USD 1.8 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu copper kwa kontena moja (6,756 kg) kiasi cha copper katika makontena 61,320 kitakuwa tani 414,278 ambazo thamani yakeni ni TZS 3,718,253,171,160 (TZS 3.7 trilioni), sawa na USD 1,690,115,078 (USD 1.6 bilioni).
Madini ya Sulphur
Kiwango cha Sulphur kilikuwa wastani wa 7,800 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na Sulphur kiasi cha tani 478,296. Kiasi hiki cha Sulphur kina thamani ya TZS 411,187,392,000 (TZS 411.18 bilioni) sawa na USD 186,903,360 (USD 186.9 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu sulphur katika kontena moja lenye uzito wa 10,160 kg, kiasi cha Sulphur katika makontena 61,320 kitakuwa tani 623,011 ambazo thamani yake ni TZS 351,675,360,000 (TZS 351.67 bilioni) sawa na USD 143,488,000 (USD 143.5 milioni).
26
Madini ya Iron
Kiwango cha iron kilikuwa ni wastani wa 5,400 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha iron kwenye kila kontena, makontena 61,320 yatakuwa na iron kiasi cha tani 331,128. Kiasi hiki cha iron kina thamani ya TZS 509,937,120,000 (TZS 509 bilioni), sawa na USD 231,789,600 (USD231 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha iron kwa kontena moja (6,100 kg) kiasi cha iron katika makontena 61,320 kitakuwa tani 374,052 ambazo thamani yake ni TZS 576,040,080,000 (TZS 576 bilioni) sawa na USD 261,836,400 (USD261 milion).
Madini ya Nickel na Zinc
Zinc
Kiwango cha zinc kilikuwa wastani wa 33.3 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na iron kiasi cha tani 2,042. Kiasi hiki cha zinc kina thamani ya TZS 11,679,988,320 (TZS 11.6 bilion) sawa na USD 5,309,086 (USD5.3 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha zinc kwa kontena moja (65.8 kg) kiasi cha zinc katika kontena 61,320 kitakuwa tani 4,035 kg ambazo thamani yakeni ni TZS 23,079,376,320 (TZS 23.1 bilioni), sawa na USD 10,490,626 (USD 10 milioni).
27
Nickel
Kiwango cha nickel kilikuwa ni wastani wa 14 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na nickel kiasi cha tani 858. Kiasi hiki cha nickel kina thamani ya TZS 18,319,963,200 (TZS 18.3 bilioni), sawa na USD 8,327,256 (USD 8.3 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha nickel kwa kontena moja 40 kg kiasi cha inickel katika kontena 61,320 kitakuwa tani 2,453 ambazo thamani yakeni ni TZS 52,342,752,000 (TZS 52 bilioni), sawa na USD 23,792,160 (USD 23.7 milioni).
Madini ya kundi la Platinum
Rhodium
Kiwango cha rhodium kilikuwa na wastani wa 0.034 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha rhodium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na rhodium kiasi cha tani 2.5. Kiasi hiki cha rhodium kina thamani ya TZS 146,461,360,584 (TZS 146 bilioni), sawa na USD 66,573,346 (USD 66.5 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha rhodium kwa kontena moja 0.078 kg kiasi cha rhodium katika kontena 61,320 kitakuwa tani 4.8 kg ambazo thamani yake ni TZS 335,999,591,928 (TZS335.9 bilioni), sawa na USD 152,727,087 (USD 152.7).
Iridium
Kiwango cha iridium kilikuwa ni wastani wa 6.4 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena
28
lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na iridium kiasi cha tani 392. Kiasi hiki cha iridium kina thamani ya TZS 23,803,540,992,000 (TZS 23.8 trilioni), sawa na USD 10,819,791,360 (USD 10.8 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha iridium kwa kontena moja 13.75 kg kiasi cha iridium katika kontena 61,320 kitakuwa tani 843 kg ambazo thamani yake ni TZS 51,140,420,100,000 (TZS 51.1 trilioni), sawa na USD 23,245,645,500 (USD 23.2).
Viwango vya Metali za Rare Earth Elements (REE), Transition Elements na Light Elements
Ytterbium
Kiwango cha tterbium kilikuwa wastani wa 3.7 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha ytterbium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na ytterbium kiasi cha tani 227. Kiasi hiki cha ytterbium kina thamani ya TZS 2,745,296,400,000 (TZS 2.7 trilioni), sawa na USD 1,247,862,000 (USD1.24 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha ytterbium kwa kontena moja 4.9 kg kiasi cha ytterbium katika kontena 301 kitakuwa tani 217 kg ambazo thamani yake ni TZS 3,635,662,800,000 (TZS 3.6 trilioni), sawa na USD 1,652,574,000 (USD 1.6 bilioni).
Beryllium
Kiwango cha beryllium kilikuwa wastani wa 19.4 kg kwenye kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena
29
lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na beryllium kiasi cha tani 1,190. Kiasi hiki cha beryllium kina thamani ya TZS 1,324,271625,600 (TZS 1.3 trilioni), sawa na USD 601,941,648 (USD 601.9 bilioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha beryllium kwa kontena moja 26.9 kg kiasi cha beryllium katika kontena 61,320 kitakuwa tani 1,650 kg ambazo thamani yake ni TZS 1,836,232,305,600 (TZS 1.8 trilioni), sawa na USD 834,651,048 (USD 834.6 milioni).
Tantalum
Kiwango cha tantalum kilikuwa wastani wa 11.7 kg kwenye kila kontena lenye tani 20, Kwa kutumia kiasi hiki kwenye kila kontena, makontena 61,320 yatakuwa na tantalum kiasi cha tani 717. Kiasi hiki cha tantalum kina thamani ya TZS 416,691,475,200 (TZS 416.6 bilioni), sawa na USD 189,405,216 (USD 189 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha tantalum kwa kontena moja 17.3 kg kiasi cha tantalum katika kontena 61,320 kitakuwa tani 1,061 kg ambazo thamani yake ni TZS 616,133,548,800 (TZS 616.1 bilioni), sawa na USD 280,060,704 (USD 280 milioni).
Lithium
Kiwango cha lithium kilikuwa na wastani wa 21.5 kg kila kontena. Kwa kutumia kiasi hiki cha lithium kwenye kila kontena lenye tani 20, makontena 61,320 yatakuwa na lithium kiasi cha tani 1,318. Kiasi hiki kina thamani ya TZS 228,264,313,200 (TZS 228.26 bilioni) sawa na USD 103,756,506 (USD 103.76 milioni). Kwa kutumia kiwango cha juu cha
30
lithium kwa kontena moja 29.8 kg, kiasi cha lithium katika kontena 61,320 kitakuwa tani 1,827 ambazo thamani yake ni TZS 316,384,955,040 ( TZS 316.38 bilioni) sawa na USD 143,811,343 (USD 143.81 milioni).
Mheshimiwa Rais
Thamani ya madini yote katika makontena 61,320 yaliyosafirishwa nje ya nchi katika kipindi kati ya 1998 na 2017 kwa kutumia kiwango cha wastani ni TZS 183,597,272,467,224 (TZS 183.597 trilioni) sawa na USD 83,453,305,667 (USD 83.45 bilioni). Jumla ya thamani ya madini katika makontena 61,320 yaliyosafirishwa nje ya nchi katika kipindi kati ya 1998 na 2017, kwa kutumia kiwango cha juu ni TZS 380,499,453,421,688 (380.499 trilioni) sawa na USD 144,772,478,828 (USD 144.77 bilioni).
Kiasi cha Mapato ambacho Tanzania Imepoteza (Kiwango cha Chini)
Chanzo
Kiasi (TZS)
kodi ya mapato ya makampuni
55,677,352,653,559
Kodi ya zuio la kodi
94,442,735,380
Mrahaba
11,147,480,869,759
Gharama za meli kutia nanga na upakuaji
1,671,281,263,923
Jumla
68,590,557,522,621
31
Jumla ya mapato ya Serikali ambayo Serikali ilipoteza ni TZS trillion 68.59 ambazo ni sawa na bajeti ya miaka miwili ya Serikali kwa kigezo cha makadirio ya mwaka 2017/2018. Aidha, robo ya fedha hizo zingetosha kujenga reli ya Standard Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
Kiasi cha Mapato ambacho Tanzania imepoteza (Kiwango cha Juu)
Chanzo
Kiasi (TZS)
Kodi ya mapato ya makampuni
95,548,006,939,893
Kodi ya zuio la kodi
94,442,735,380
Mrahaba
11,147,480,869,759
Gharama za meli kutia nanga na upakuaji
1,671,281,263,923
Jumla
108,461,211,808,955
32
Jumla ya mapato ya ambayo Serikali ilipoteza ni TZS trilion 108.46, ambazo ni sawa na bajeti inayokaribia Miaka Mitatu ya Serikali kwa kigezo cha Makadirio ya Matumizi ya mwaka 2017/2018 na gharama ya kujenga reli ya Standard Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
4. Taarifa za Uchenjuaji Makinikia Nje ya Nchi
Mheshimiwa Rais
Kamati imepata na kusom mikataba ya mauzo ya makinikia kati ya makampuni ya uchimbaji na wachenjuaji. Katika mikataba hiyo, Serikali siyo sehemu ya mikataba hiyo icha ya kuwepo na salio la kodi katika makinikia hayo.
Aidha, mikataba hiyo haina masharti yanayozilazimu kampuni za uchenjuaji kutoa taarifa za uchenjuaji kwa Serikali au muuzaji.
33
Kwa msingi huo, taarifa ambazo zimekuwa zikiwasilishwa kwa TMAA baada ya kuomba taarifa hizo kutoka makampuni ya madini hazina ukweli na hazibebi takwimu sahihi kuhusu aina, kiasi na thamani ya madini yaliyochenjuliwa ambazo zingewezesha TRA kutoza kodi stahiki.
5. Mikataba ya uchimbaji madini (Mining Development Agreements-MDAs)
Mheshimiwa Rais,
Mikataba ya uchimbaji wa madini inafanyika chini ya kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini, Sura 123. Kwa mikataba iliyoingiwa mwaka 1994, mikataba hiyo ilifanyika chini ya kifungu cha kifungu 15 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1979 na kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 .
Mikataba mikubwa ya madini ni kama ifuatavyo:
i. Mgodi wa Bulyanhulu Gold Mines Ltd (Kahama Mine Corporation Limited).
Katika mkataba huu, Waziri wa Nishati na madini kwa jitihada kubwa alifanikiwa kujadiliana na kampuni hii na kuiwezesha Serikali kupata asilimia 15 za hisa katika
34
kampuni za uchimbaji Hata hivyo, mkataba huo ulifanyiwa marekebisho mwezi Juni, 1999 na kusainiwa na Waziri wa Nishati na Madini aliyefuata, Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda. Marekebisho hayo yaliondoa asilimia 10 ya hisa ambazo Serkali ilikuwa inamiliki na kubakiza asilimia 5 tu. Marekebisho mengine katika mkataba huo huo yalifanyika Oktoba, 1999, ikiwa ni miezi minne tu tangu marekebisho ya awali yafanyike. Marekebisho haya ya pili pia yalitiwa saini na Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda , ambayo yaliondoa asilimia 5 ya hisa za Serikali zilizokuwa zimebakia na hivyo, Serikali kubaki bila hisa yoyote. Katika marekebisho hayo, Serikali ilikubali kulipwa USD 5,000,000 ikiwa ni malipo ya mauzo ya hisa za Serikali.
Aidha, Serikali ilikubali kuendelea kulipwa kiasi cha USD 100,000 kwa kila mwaka. Hata hivyo, Kamati haikuweza kupata uthibitisho wa kufanyika kwa malipo ya jumla ya USD 6,800,000.
Kamati imeona kwamba marekebisho hayo ya mkataba yaliyofanywa na Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda hayakuwa na maslahi kwa taifa kwani Serikali ilipoteza haki ya umiliki wa hisa na kuinyima mapato kutokana na gawio (dividend).
35
ii.
Pangea Gold Mine Ltd
Kampuni hii ina mikataba miwili ya uchimbaji madini. Mikataba wa kwanza ulisainiwa Disemba 2003 na Mheshimiwa Daniel N.Yona akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Mkataba wa pili ulisainiwa na Mheshimiwa Nazir M. Karamagi akiwa Waziri wa Nishati na Madini.Katika mikataba hii yote Serikali haina hisa yoyote katika kampuni na pia mkataba huu unatoa nafuu kubwa sana za kodi kwa kampuni, jambo ambalo lina ikosesha Serikali kodi nyingi na mapato.

North Mara Gold Mine Ltd ,
Mkataba huo ulisainiwa Juni 1999 na Mheshimwa Daniel N.Yona, akiwa Waziri wa Nishati na Madini na baadaye, marekebisho ya mkataba huo yalifanywa mwaka 2007 na Mheshimiwa Nazir M. Karamagi akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Katika mkataba huo Serikali haina hisa yoyote katika kampuni. Aidha katika mkataba wa awali, uliotiwa saini na Mheshimiwa Daniel N. Yona, Serkali ilitoa nafuu ya asilimia 15 ya nyongeza ya mtaji wa kampuni (additional capital allowance), na kuifanya kampuni hiyo iwe inajilipa kwanza ili kurudisha mtaji wake na asilimia 15 iliyopewa na Serikali na hivyo kusababisha kampuni kutangaza hasara katika biashara kila mwaka. Jambo hilo limekuwa linaikosesha Serikali kodi ya mapato. Kamati imebaini kwamba marekebisho yaliyofanyika mwaka 2007
iii.
36
kuondoa nafuu ya asilimia 15, bado malimbikizo ya hasara kutokana na nafuu ya kodi iliyokuwa imetolewa na Serikali iliendelea kudaiwa na kampuni hii.
iv. Geita Gold Mine Ltd (AngloGold Ashanti Ltd);
Mkataba huu ulisainiwa na mheshimwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Katika mkataba huu Serikali haikupata hisa yoyote katika kampuni na pia mkataba huu unatoa nafuu mbali mbali za kodi kwa kampuni, jambo ambalo lina ikosesha Serikali kodi nyingi na mapato.
Mikataba ya uchimbaji madini inaeleza kuwa inaongeza na kurekebisha masharti yaliyomo katika leseni za uchimbaji madini. Kamati inaona kuwa masharti ya aina hiyo ni batili kisheria kwani Waziri hawezi kurekebisha masharti ya leseni yaliyotolewa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni kwa kupitia vifungu vya mkataba wa uchimbaji wa madini.

Aidha, Kamati imebaini kuwa kumekuwa na uongezaji wa muda wa leseni (renewal) wa maeneo ya uchimbaji madini kinyume cha sheria na bila kuzingatia maslahi ya taifa.Kwa mfano, kuongeza muda wa leseni na maeneo ya uchimbaji uliofanywa na Mheshimiwa William M. Ngeleja na Mheshimiwa Sospeter M. Muhongo, kwa kampuni za North Mara Gold Mines limited na Pangea Minerals Limited.Pia
37
leseni mbali mbali zilizotolewa na; Kamishna Paulo M. Masanja, Kamishna Dalaly P. Kafumu na Kaimu Kamishna Ally B. Samaje. Katika kipindi hicho washauri wakuu wa Serkali kwa masuala ya kisheria ni pamoja na Mheshimiwa Andrew Chenge, Johnson Mwanyika na Manaibu Wanasheria Wakuu ambao ni Felix Mrema na Sazi Salula na Wakuu wa Idara ya Mikaba Maria Ndossi Kejo na Julius Malaba.
b. Kifungu thabiti (stability clause)
Mikataba ya uchimbaji madini ina vifungu dhabiti ambavyo vinazuia marekebisho ya sera na sheria kuathiri masharti yaliyomo katika mikataba ya uchimbaji madini. Kamati iliona kuwa pamoja na uwepo wa vifungu thabiti, Serikali haizuiliwi kurekebisha au kubadili Sera na Sheria zinazoweza kuathiri mikataba ya uchimbaji madini. Aidha, mkataba wowote ule hauwezi kisheria kuwa juu ya Mamlaka asili ya Nchi (state soveregnity) na maslahi ya umma kuhusu raslimali zake za asili.
Pia, mikataba hiyo ina vifungu vinavyoruhusu Serikali na makampuni ya uchimbaji kujadili na kurekebisha sharti lolote la kimikataba. Hivyo, mikataba ya uchimbaji madini inaweza kurekebishwa. Ipo mifano mingi inayoonesha kuwa masharti yenye vifungu dhabiti haiondoi mamlaka ya nchi kufanya maamuzi ya kisera
38
au sheria ambayo yana maslahi kwa taifa na wananchi wake. Kila nchi inayo kusimamia kanuni ya umiliki wa milele wa mali asili yake kwa mujibu wa azimio Na. 1803 la mwaka 1962 la Baraza kuu la Umoja wa mataifa, Azimio Na. 3281 la 1974 la Baraza kuu la Umoja wa Mataifa la Haki na Majukumu ya Kiuchumi ya Mataifa. Maazimio yote yanatamka bila shaka haki na mamlaka ya nchi kuweka mifumo ya kuondoa unyonyaji katika maliasili na kuamua migogoro juu ya mali asili ikiwemo madini, gesi na mafuta.
c. Misamaha ya kodi
Mikataba ya uchimbaji madini ina vifungu vingi vinavyotoa misamaha mingi ya kodi ambayo haina maslahi kwa taifa. Kwa kutumia mikataba hiyo, makampuni yamekuwa hayalipi kodi kwa kutumia kinga hiyo. Inatosha kusema kuwa mikataba hii haina manufaa kwa Taifa.

d. Utunzaji na uhamishaji wa fedha katika mabenki Mikataba ya uchimbaji madini inaruhusu kuweka na kuhamisha fedha zinazotokana na mauzo ya madini nje ya nchi. Kamati imeona kuwa hali hiyo inainyima nchi nafasi ya kukuza uchumi, kuongeza thamani ya fedha yake kutokana na mauzo ya madini kwa sababu fedha haziwekwi katika mabenki yaliyomo ndani ya nchi.
39
Aidha, kamati inaona kuwa utaratibu wa kuweka fedha katika mabenki ya ndani ungewezesha kupunguza mianya ya ukwepaji kodi unaofanywa na makampuni ya madini. Ni wakati sasa nchi yetu ikaachana na uhuru ambao makampuni ya migodi yamepewa ya kuhifadhi fedha zitokanazo na madini nje ya nchi. Ofisi za mauzo pia sharti ziwepo nchini na siyo nje ya nchi.
  1. Ajira na mafunzo kwa Watanzania
    Mikataba ya uchimbaji madini ina zitaka kampuni za madini kuajira kuwaendeleza wazawa kimafunzo ili waweze kupata ujuzi na kuwa waendeshaji wakuu wa shughuli za uchimbaji madini katika makampuni hayo badala ya kuwaajiri watu wa nje.

    Kamati imebaini kuwa hakuna utaratibu madhubuti uliowekwa na Serikali katika kutimiza azma hiyo juu ya mafunzo na ajira kwa wazawa. Kamati imeona kwamba Tanzania inaweza kujifunza kutoka nchi ya Ghana ambayo imeweka sharti la kuonyesha utaratibu wa kipindi maalum cha mafunzo na ajira kwa wazawa kama kigezo mojawapo muhimu kabla ya kampuni ya uchimbaji madini kupewa leseni.
  2. Uwajibikaji katika utoaji huduma kwa jamii
40
Mikataba ya uchimbaji madini inazitaka kampuni za uchimbaji madini kushiriki na kuchangia kikamilifu shughuli za maendeleo katika jamii inayowazunguka. Kamati iliona taarifa za uchangiaji wa shughuli hizo za maendeleo kwa jamii. Hata vivyo, uchangiaji huo ni mdogo mno kulingana na mapato ya makampuni hayo.
Kamati inaona ni vyema sheria ikaweka kiwango maalum cha asilimia ya mapato inayotakiwa kuchangiwa katika shughuli za maendeleo ya jamii.
  1. Uhuru wa madaraka aliyo nayo Waziri (discretionary powers)
    Sheria ya Madini inatoa uhuru wa madaraka ya Waziri katika kuingia katika mikataba ya madini na mambo mengineyo. Kamati inaona kuwa madaraka hayo yanapaswa kudhibitiwa na mikataba yote mikubwa ya madinin inapaswa kupata idhini nya Bunge (ratified by National Assembly/Parliament) kama nchi nyingine kama Ghana inavyofanya.
  2. Ushiriki wa Serikali katika uchimbaji wa madini
    Kamati ilisoma sheria ya Madini na kuona kuwa haitoi nafasi ya ushiriki wa Serikali katika umiliki wa hisa katika makampuni ya uchimbaji madini. Kutokana na hali
41
hiyo kamati inaona kuna haja kuwa kifungu katika Sheria ya madini kinachoweka kiwango maalum cha asilimia ya hisa ambazo zitamilikiwa na Serikali katika makampuni yote ya madini nchini. Aidha Sheria itoe hiari kwa Serikali kupata hisa nyingine kutoka kwa makampuni ya madini nje ya asilimia itayowekwa na Sheria kwa makubaliano na makampuni. Umiliki wa hisa utaiwezesha Serikali kupata mapato na ushiriki katika maamuzi muhimu katika biashara ya madini.
8. Kamati imeona hakuna sababu ya kupeleka migogoro nje ya nchi kwa ajili ya usikilizwaji na uamuziikiwa wahisika katika mikataba hiyo wote ni watanzania na migodi ipo Tanzania. Aidha, kuna mahakama kuu ya Tanzania, kitengo cha Biashara ambayo ipo kwa ajili ya migogogoro kama hiyo. Kwa hiyo mahakama zetu zitumike kutatua migogoro hiyo.
9. Kiwanda cha Uchenjuaji wa Makinikia
Tanzania inaweza kuanzisha na kuendesha kiwanda cha kuchenjua makinikia kwa kuzingatia kuwa teknolojia iliyopo ndani inayopatikana nje ya nchi zinaweza zikatumika; mtaji unaweza kupatikana kwa kutumia vyanzo vya ndani na mikopo; malighafi inaweza kupatikana toka migodi ya ndani na kutoka nchi jirani zinazochimba madini kama vile Zambia, na Jamhuri ya Kidemikrasia ya Kongo.
42
  1. Taasisi zenye Dhamana ya Kusimamia Sekta ya Madini
    Tanzania ina taasisi nyingi zenye dhamana ya kusimamia uendeshaji wa sekta ya madini pamoja na ukadiriaji na ulipaji wa kodi za Serikali. Hata hivyo, kwa bahati mbaya sana kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi sana kwenye sekta ya madini kutokana na wizi na udanganyifu unaofanywa na makampuni ya uchimbaji madini, watumishi wenye tamaa na kujali masilahi binafsi na taasisi zinazosimamia uendeshaji wa sekta ya madini kushindwa kusimamia vyema sekta ya madini.
  2. Ukosefu wa Wakala wa Meliwa Serikali Mheshimiwa Rais
    Nchi yetu imekuwa inapoteza mapato mengi sana kupitia bandari zetu kwa kuwa Serikali haina wakala wa meli ambaye angeweza kusimamia usafirishaji wa mizigo nje kwa njia ya meli pamoja na biashara zingine zote zinazohusiana na usafirishaji wa mizigo nje kwa meli. Utaratibu huu ungeisaidia Serikali kwa kiwango kikubwa kwa kuratibu na kuhakikisha mapato yote yatokanayo na biashara hizi yanalipwa Serikali Kuu. Sasa hivi, na hasa baada ya kuvunjwa kwa Wakala wa Meli Tanzania (NASACO), biashara karibu zote
43
zinamilikiwa na kuendeshwa na wenye meli, ambao wana ridhaa ya kupanga bei na hata kujilimbikizia mapato ambayo yangestahili kwenda Serikalini.
Mapato mengi ya Serikali yanapotea kwa kutokuwa na Wakala wa Meli wa Serikali; makadirio ya chini (kwa makusudi) ya mirahaba; udanganyifu katika upimaji wa kimaabara wa madini unaofanywa na TMAA na SGS;
Mapendekezo
Mheshimiwa Rais,
Kutokana na uchunguzi, Kamati Maalum imebaini kuwa kuna ukiukwaji wa sheria za nchi na upotevu mkubwa wa mapato ya Serikali kupitia biashara ya Makinikia na madini yanayosafirishwa nje ya nchi. Kamati hii inatoa mapendekezo kwa Serikali kama ifuatavyo:
  1. Serikali, kupitia Msajili wa Makampuni ichukue hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Acacia Mining Plc ambayo imekuwa inaendesha shughuli zake nchini kinyume na matakwa ya Sheria.
  2. Serikali idai kodi na mrahaba kutoka kwa makampuni yote ya madini ambayo yamekwepa kulipa kodi na mrahaba stahiki kwa mujibu wa sheria.
44
  1. Serikali iendelee kuzuia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi mpaka hapo makampuni ya madini yanayodaiwa yatakapolipa kodi, mrahaba na tozo stahiki kwa mujibu wa sheria.
  2. Serikali ianzishe utaratibu utakowezesha ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji wa makinikia (smelter) ili kuondoa upotevu wa mapato na kutengeneza ajira kwa watanzania.
  3. Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waliokuwa Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali na Manaibu wao, Wakurugenzi wa idara za mikataba, na Makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wengine wa Serikali na watu wote waliohusika katika kuingia mikataba ya uchimbaji madini, utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini na kuongeza muda wa leseni, watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini, makampuni yaliyohusika kuandaa nyaraka za usafirishaji wa makinikia(Freight Forwarders(T)Ltd na makampuni ya upimaji wa madini kwa kuvunja sheria za nchina upotoshaji.
  4. Serikali ifute utaratibu wa kupokea malipo ya mrahaba ya asilimia 90 na kusubiri malipo ya asilimia 10 kulipwa
45
baadaye wakati makampuni hayo ya madini huyauza madini hayo na kupewa fedha taslimu kwa mkupuo.
7. Serikali ifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa Watumishi wa idara ya walipakodi wakubwa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kushughulikia madai ya kodi ambayo Mabaraza ya Rufaani ya Kodi na Mahakama zimekwisha yatolea uamuzi na vilevile ichunguze mienendo ya watumishi wa mabaraza ya Kodi kwa kutotolea maamuzi ya kesi za kodi kwa muda mrefu kuhusu mashauri yaliyochukua muda mrefu kukamilika katika vyombo hivyo.
  1. Benki Kuu ya Tanzania ifuatilie malipo ya fedha za kigeni yanayotokana na mrahaba kwa mauzo ya madini.
  2. Serikali ianzishe utaratibu wa kulinda maeneo ya migodi na viwanja ndege vilivyopo vigodini ili kudhibiti vitendo vya hujuma vinavyoweza kuwa vinafanywa na makampuni ya migodi ikiwemo utoroshaji wa madini.
  3. Sheria iongeze kiwango cha adhabu zilizoainishwa kwa makosa ya ukiukwaji wa Sheria ya Madini na Sheria za Kodi.
46
  1. Serikali kupitia wataalum wabobezi katika majadiliano na mikataba (expert in negotiation and contract) wapitie mikataba yote mikubwa ya uchimbaji madini ipitiwe (review) na kufanya majadiliano na makampuni ya madini ili kuondoa misamaha yote ya kodi isiyokuwa na tija kwa taifa na badala yake kuweka masharti yenye tija kwa pande zote mbili kwa kuzingatia maslahi ya nchi;
  2. Sheria iweke kiwango maalum cha asilimia ya hisa ambazo zitamilikiwa na Serikali katika makampuni yote ya madini nchini. Aidha, Sheria ielekeze Serikali kufanya majadilaino ili kuwezesha Serikali kununua hisa katika makampuni ya uchimbaji madini ili kuiwezesha kupata mapato zaidi na ushiriki katika maamuzi muhimu katika biashara ya madini.
  3. Serikali iunde chombo cha kusimamia biashara ya usafirishajibidhaa nje ya nchi kupitia bandari kama ilivyokuwa kama lilivyokuwa shirika la NASACO ili kudhibiti biashara haramu na kuondoa mianya ya ukwepaji kodi.
  4. Sheria itamke bayana kuwa madini ni mali asili ya watanzania na iwekwe chini ya udhamini na uangalizi wa Rais kwa manufaa ya watanzania.
47
  1. Sheria itamke bayana kuwa mikataba yoyote ya uchimbaji mkubwa wa madini (Mining Development Agreement) isiwe ya siri na lazima yaridhiwe na Bunge kabla ya kuanza kutekelezwa.
  2. Sheria itoe masharti ya wazi ya kuzingatiwana iondoe uhuru wa mamlaka ya (discretionary powers) za Waziri wa Nishati na Madini, kamishna wa madini na maafisa madini wakanda katika utoaji wa leseni za uchimbaji madini.
  3. Sheria ya madini iweka masharti kwamba mwombaji wa leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini lazima yaoneshe mchanganuo wa kina kuhusu namna mafunzo kwawazawa yatakavyotolewa kwa lengo la ajiri kama wataalam na kuchukua nafasi za uendeshaji wa migodi husika na kupunguza au kuondoa kabisa wataalam kutoka nje ya nchi.
  4. Sheria ielekeze makampuni ya madini kuweka fedha zinazotokana na mauzo ya madini katika benki zilizopo nchini ili kuimarisha uchumi wa nchi na kuondoa mianya ya ukwepaji wa kodi na tozo mbalimbali.
  5. Serikali ipitie na kufanya marekebisho au kufuta na kubadili kabisa Sheria ya Madini na Sheria za Kodi ili kuondoapamoja mambo mengine masharti yote
48
yasikuwa na manufaa kwa taifa ikiwa ni pamoja na masharti yaliyomo kwenye kifungu thabiti (stability provision).
  1. Serikali igharimie nakutoa mafunzo kwa watumishi wa Serikali ili kuwapatia uelewa na weledi katika nyanja ya majadiliano na uendeshaji wa mashauri yatokanayo na mikataba ikiwemo ya mikataba ya madini (skills in negotiation and arbitration).
  2. SerikalikupitiaKamishnawaMadiniiweinafanyaukaguzi wa mara kwa mara kaw makampuni ya madini ili kujihakikishia uzingatia au ukiukwaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji na kuchukua hatua ipasavyo.
Mheshimiwa Rais,
Kwa mara nyingine tena mimi binafsi na kwa niaba ya wajumbe wa kamati maalum, nakushukuru kwa imani yako kwetu.
Kwa heshima kubwa, naomba kuwasilisha.
49


No comments:

Post a Comment