Thursday, April 06, 2017

MD KAYOMBO ATEMBELEA OFISI YA MTENDAJI KATA YA UBUNGO

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Ofisi Mtendaji wa Kata ya Ubungo, kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kata Ya Ubungo Ndg Isihaka Waziri
 
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo April 6, 2017 amefanya ziara katika Ofisi ya Ofisa Mtendaji Kata ya Ubungo ili kujionea utendaji kazi katika Ofisi hiyo.

Akizungumza na baadhi ya watumishi Mara baada ya kukagua eneo la Ofisi hiyo MD Kayombo Alisema kuwa amefanya ziara hiyo ya kushtukiza ili kujionea hali ya ufanisi wa kazi na kubaini kama kuna watumishi ambao hawafanyi kazi ya kuwatumikia wananchi kwa weledi na badala yake wanafika ofisini Asubuhi kwa ajili ya kusaini na hatimaye wanaondoka.

"Watumishi wengi hutumia muda mwingi kufanya kazi zao badala ya kufanya kazi za utumishi wa wananchi, Japo nawapongeza katika Ofisi hii mmeendelea kuwa waumini wazuri wa kazi na ufanisi wenu unawasaidia wananchi kuzidi kuiamini serikali yao" Alisema MD Kayombo


Akiwa Ofisini hapo MD Kayombo ameagiza Marobota ya vyandarua zilizobaki ambazo zilitolewa kwa ajili ya kuwagawia wananchi kutotolewa hovyo ama kuhamishwa badala yake zitolewe kwa utaratibu mahususi utakaoelekezwa na Ofisi ya Mkurugenzi.

Robota hizo zipo 34 katika Ofisi hiyo ya Mtendaji wa Kata ya Ubungo zimesalia nyingi kutokana na wananchi wengi kutojitokeza kuzichukua kutokana na sababu mbalimbali.

MD Kayombo pia ameelezea mpango kabambe wa Manispaa ya Ubungo juu ya Ofisi hiyo ya Mtendaji kubomolewa na hatimaye kuwa na uwekezaji mkubwa ambao utaongeza wigo wa ukusanyaji mapato ya Manispaa hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa maelekezo kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ubungo kuhusu namna ya kuyatoa marobota yaliyobaki baada ya kuwagawia wananchi vyandarua
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiongea na baadhi ya watumishi aliowakuta ofisini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua eneo La Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ubungo Mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo



No comments:

Post a Comment