Tuesday, February 21, 2017

SBL YAANZA KUUZA BIA KENYA

Dar es Salaam, Februari 20, 2017- Kwa mara ya kwanza, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imeanza kuuza nje ya nchi bidhaa zake katika soko la kikanda, eneo la kwanza likiwa ni nchi jirani ya Tanzania kwa upande wa Kaskazini, Kenya.

Shehena ya kwanza ya bia inayofahamika kama Allsopps ilisafirishwa kwenda Kenya wiki iliyopita na hivyo kukiweka kiwanda cha SBL kuwa mmoja wachangiaji wakubwa katika soko la kanda.

Akizungumzia kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha alisema; “Hii ni hatua nyingine ya kufurahisha katika kampuni yetu na kimsingi kwa bidhaa zetu. Ukweli unabakia kwamba kumudu kupenyeza ndani ya soko la Kenya kunaonesha kuwa ubora wa bidhaa zetu sio tu kwamba unakubalika na wateja wetu wa ndani bali pia zinakubalika katika soko kubwa la kikanda.”

Wanyancha alisema kuwa SBL inaangalia uwezekano wa kupanua mauzo ya biashara katika masoko mengine ya kikanda, hatua ambayo iko katika mkondo wa kuhamasisha Jumuia ya Afrika Mashariki na kada nyingine za kiuchumi kuongeza biashara yake ya kuvuka mpaka ndani ya ukanda huo.

SBL imekuwa inazalisha aina za bidhaa zinazotambulika kimataifa kama vile Pilsner Lager,Tusker Lager, TuskerLite, Kibo Gold, Guinness Stout, Uhuru, The Kick pamoja na bidhaa kuu ya Serengeti Premium Lager-ambayo peke yake imeshajizolea medali kumi zinazotambuliwa kimataifa.



No comments:

Post a Comment