Thursday, January 05, 2017

MHARIRI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA WIZI WA GARI

Na Mwandishi Wetu

Mwandishi na Mhariri wa shirika la Standard Media Group nchini Kenya Aaron Ochieng(Pichani Kushoto) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa gari lenye thamani ya shilingi za Kenya milioni 2.8 sawa na shlingi za Tanzania milioni 58.5

Mwandishi huyo ambaye pia ni Mhariri, amefikishwa katika Mahakama ya Nairobi baada ya kukutwa na gari aina ya Mercedes Benz E-220 (Pichani katikati) eneo la Kisumu, mali ya mfanyakazi mwenzie Joy Doreen Biira(Pichani kushoto), tukio la wizi lilitokea tarehe 23 disemba 2016.katika barabara ya Mombasa.

Kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa CitizenTv, iliyochapishwa tarehe 3 january, 2017. Ochieng ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja ya Kenya (sawa na Shilingi milioni 20.9) au fedha taslimu shilingi 300,000 za Kenya (sawa na shilingi 6,270,000 za Tanzania). Ochieng alikamatwa tarehe 31/12/2016 ambapo hakimu alimtaka wakili wa mwandishi huyo, Ken Bosire, kuwasilisha hati ya ushahidi au hati nyingine yeyote kabla ya kusikilizwa kwa kesi hiyo itakayosikilizwa tarehe 3 mwezi februari, 2017.

Pamoja na Ochieng, walinzi wawili waliokuwa lindoni siku ya tukio pia wanashikiliwa katika kituo cha polisi cha Makadara wakati upelelezi unaendelea



No comments:

Post a Comment