Thursday, December 01, 2016

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU ANUSURIKA KUFA MARA BAADA YA KUBWAKWA NA KUTELEKEZWA KORONGONI



Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo
Na Woinde Shizza,Meru

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu iliyopo Meru mkoani Arusha amenusurika kufa mara baada ya kubakwa na kuteketezwa kwenye korongo la mchanga na kusababishiwa maumivu makali yaliyomsababishia kushindwa kuendelea na masomo yake kwa muda.

Akielezea tukio hilo mwanafunzi huyo ambae amehifadhiwa jina kwa sababu za kimaadili alisema kuwa tukio hilo lilitokea novembar 13 majira ya saa 12.30 alipotoka kwa kinyozi.

Alisema kuwa ghafla akiwa anarudi nyumbani alikutana na mtu huyo aliyemfanyia kitendo hicho na kuanza kumkaba shingoni na kumziba mkono ili asitoe sauti na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili ambacho kimemfanyia ashindwe kuendelea na masomo yake vizuri.

"Nilijitahidi sana kupiga kelele ila kutokana na alivyokuwa amenikaba shingoni alinifanyia kitendo hiki kikatili ambacho kimejipelekea nishindwe kuendelea na masomo yangu kwani baada ya vipimo nimeonekana aliniumiza sehemu nyingi ikiwemo hata kifua changu"alisema mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake mama mzazi wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha Rambikiaeli Akyoo alisema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili kukithiri kwa mabinti zao ni vema serikali ikawa inawachukulia hatua mapema wanaohusika kwani tangu akamatwe mtuhumiw huyo na kupellekwa kituoni bado hajasomewa shtaka linalomkabili hivyo kufanya wanaohusika na vitendo hivyo kuona wako sawa kwa vile hakuna hatua kali inayochukuliwa mapema dhidi ya matukio hayo

Nae mkuu wa shule hiyo Nkoe Nicolaus alisema kuwa tukio hilo limemfanya mwanafunzi huyo aathirike kisaikolojia kwani tangu afanyiwe ukatili huo ameshindwa kiendelea na masomo yake vizuri hivyo anawashauri wazazi wa binti huyo kumuhamisha shule hiyo na kumuhamishia nyingine ili kimbadilisha mawazo ya kifkra.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kitefu tanesco Samweli Matayo alikiri kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake na kusema kuwa mara baada ya taarifa walifanikiwa kumtia hatiani mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Wilson Elias ambae ndie aliyehusika na ukatili huo na kumfikisha katika kituo kidogo cha polisi usa river ili kukabiliana na shutuma hizo.

Kamanda wa polisi Charles Mkumbo amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambapo limesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa kwa rb namba RB/R/4250/2016 na atafikishwa
mahamani upelelezi ukikamilika.


No comments:

Post a Comment