Tuesday, June 28, 2016

TANAPA YATOA MILIONI 600 KUSAIDIA VIKUNDI 70 VYA MWAMBAO MWA ZIWA TANGANYIKA VINAVYOZUNGUKA HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA YA MAHALE

Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale,Romanus Mkonda akitoa maelezo mafupi mbele tya waandishi wa habari waliotembelea vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo iliyopo mkoani Kigoma.
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda akizungumza na wananchama wa vikundi vya kijasiliamali vinavyojulikana kama COCOBA vinavyosaidiwa na hifadhi hiyo (hawapo pichani.
Baadhi ya wanachama wa vikundi wakiwa katika mkutano na watumishi wa TANAPA pamoja na wanahabari waliotembelea vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mlima ya Mahale .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ,(TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza katika mkutano huo ,kulia kwake ni Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda.
Baadhi ya Wanahabari walioitembelea vijiji hivyo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Katumbi ,Issa Zuber ,kijiji kimojawapo ambacho wanachi wananufaika na msaada wa mafunzo ya ujasiliamali unaotolewa na TANAPA,
Mwenyekiti wa Kikundi cha Mshikamano ,Juma Makumbi akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale akiteta jambo na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,Tanzania ,Pascal Shelutete mara baada ya kuzungumza na wanachama wa vikundi vinavyopewa msaada na shirika hilo .



Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.

Wananchi wa vijiji vya Buhungu na Konkwa vilivyoko mwambao mwa ziwa Tanganyika wilaya Uvinza mkoani Kigoma wanalazimika kuhifadhi mamilioni ya fedha za miradi ya vikundi vyao kwenye masanduku ya chuma na kuyafukia chini ya ardhi kutokana na ukosefu wa huduma za taasisi za fedha utaratibu waliodai kuwa unaotishia usalama wa fedha hizo na pia maisha yao .

Wananchi hao pamoja na kuwashukuru wadau wanaowasaidia likiwemo Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia Hifadhi yake ya Milima ya Mahale wamesema wanatumia njia hiyo kutokana na kuogopa kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha umbali mrefu ili kuzifikia taasisi za fedha zilizoko kigoma mjini na wameiomba serikali na asasi za fedha kusogeza huduma katika maeneo ya vijijini.

Mkufunzi mkuu wa vikundi vya benki ya jamii ya uhifadhi (COCOBA) vinavyo fadhiliwa na shirika la hifadhi za taifa (TANAPA), Simada Andrea amesema kuwa vikundi hivyo vinavyoizunguka hifadhi ya milima ya mahale, vina sifa za kupewa mikopo lakini benki zimekuwa zikiwakataa na kuwapa masharti magumu.

“Sifa za kupewa mikopo wanazo…tatizo benki zinakataa kuwakopesha kwa sababu ya umbali, zinawataka watu wa mijini kwa madai kuwa wataweza kuwafuatilia,” alisema.

Alisema vikundi hivyo, vimesajiliwa na serikali za vijiji na halmashauri ya wilaya ya uvinza iliwahi kuvikopesha kwa majaribio sh. milioni 3 na vikarudisha kwa wakati.

“Naomba niziambie benki kuwa vikundi vya cocoba vinakopesheka na vinalipa kwa wakati,” alisema.


Hata hivyo, Andrea aliziomba taasisi hizo za kifedha kupeleka huduma katika maeneo yao ili ziwawezeshe kufanya shughuli zao kwa urahisi na kwa uhuru hatua itakayowaongezea tija na ufanisi.

Naye, afisa mtendaji wa kijiji cha Nkonkwa, Issa Fungameza alisema kuna vikundi hivyo kwa sasa vinatunza fedha zao katika kiboksi cha chuma kutokana na benki kuwa mbali.

“Vikundi vinakopesheka, kwa kuwa benki ziko mbali hivyo wanashindwa kupeleka fedha hizo benki na kuamua kuzitunza kwenye kiboksi cha chuma,” alisema.

Fungameza aliiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa undani zaidi kwa kuvikopessha vikundi hivyo ili viweze kujiinua kiuchumi na kimaendeleo.

Mkuu wa idara ya ujirani mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Mahale,Romanus Mkonda alisema TANAPA imetoa zaidi ya milioni 600 kuvisaidia vikundi zaidi ya 70 vya wananchi katika vijiji hivyo kupata mafunzo ya ujasiria mali , uhifadhi wa mazingira na mitaji, hatua inayolenga kuwaepusha wananchi hao kujihusisha na uharibifu wa mazingira na ujangili katika maeneo yaliyohifadhiwa ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale


















No comments:

Post a Comment