Friday, May 06, 2016

MWAKYEMBE:UBAKAJI UMEZIDI KUWA TISHIO KWA WATANZANIA

Serikali imekiri kuwa sasa vitendo vya kubaka na kulawiti vimefikia mahali pabaya ambapo matukio 19 kwa siku yamekuwa yakiripotiwa nchini.
Pia katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huujumla ya mashauri 2,031 yaliripotiwa.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe amesema hayo leo Bungeni alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa viti maalum,Angelina Malembeka (CCM).Katika swali lake Malembeka aliuliza kuhusu vitendo vya kubaka na kulawiti ambavyo vimekuwa vikijirudia mara kwa mara na pia katika kipindi kilichopita hadi sasa kesi ngapizimepelekwa mahakamani.
“Kwa kuwa adhabu moja wapo ni kifungo cha maisha kwa wale wanaopatikana na hatia na gerezani wamekuwa na tabia kama hiyo,serikali haioni kwamba kwa kuwaweka gerezani maisha wataendelea
kufanya hivyo kwanini adhabu isiongezwe waweze kuhasiwa?,”alihoji Malembeka.
Akijibu swali hilo, Mwakyembe amesema hivi sasa matukio hayo yameongezeka kwa kiasi kikubwa licha ya uwepo wa adhabu kali kwa wanaobainika kufanya hivyo.
“Katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu jumla ya mashauri 2,013 yameripotiwa na hadi sasa mahakama mbalimbali nchini zimekamilisha kesi 111 za matukio hayo,”anasema Mwakyembe.
Pia amesema kuwa watuhumiwa 96 walihukumiwa vifungo na wengine 18 waliachiwa huru kwa kukosa ushahidi.
Hata hivyo amesema hawezi kuwa na jibu kwakuwa Bunge ndilo linalotunga sheria Mbunge aende na wazo hilo la kuwahasi ili wabunge waweze kupitisha.
Dkt. Mwakyembe akijibu swali la msingi, amesema ili kuweka mazingira rafiki kwa waathirika na wananchi wenye taarifa au ushahidi wa aina hiyo , serikali imeanzisha madawati ya jinsia katika vituo mbalimbali
vya Polisi.
Anaendelea kuwa kwa utaratibu huo Serikali inahakikisha kuwa matukio hayohayamalizwi kifamilia au nje ya utaratibu wa kijinai.
Katika swali lake la msingi mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kuwa kesi hizo hazimalizwi kifamilia na matukio ya kubakwa na kulawitiwa kwa watoto yamekuwa yakijitokeza na
kuripotiwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.


No comments:

Post a Comment