Friday, May 20, 2016

CHINA YAKANUSHA KUPELEKI NYAMA YA BINADAMU AFRIKA


Na Mwandishi Wetu

Balozi wa China nchini Zambia ametoa taarifa jumanne wiki hii yenye lengo la kupambana na ‘uzushi’ unaochafua hadhi ya nchi yake barani Afrika. “Hii ni kashfa isiyokubalika yenye lengo la kuchafua,” kwa mujibu wa taarifa ya Yang Youming, ambayo imepingwa katika vyombo vya habari nchini China.

Kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo, Uongo huo umedai kuwa Wachina husindika nyama ya ya watu waliokufa, kisha kuleta Afrika katika masoko (Supermarkets).
------------------------------------------------------
PICHA KULIA: Taarifa ikisambazwa katika mitandao ya Jamii.
-----------------------------------------------------
Vyombo vya habari nchini China vimelalamikia magazeti ya Zambia kwa kusambaza uzushi huo na kudai kuwa “Watu wenye malengo mabaya wana nia ya kuharibu uhusiano wa muda mrefu kati ya China na Zambia.” Imedaiwa kuwa uzushi huo ulisambaa zaidi katika mitandao mbalimbali ya jamii ikiwemo ya Facebook na blog.

Taarifa ziliwakariri baadhi ya watu waliowahi kuishi na kufanya kazi katika viwanda vya kusindika nyama nchini China, wakidai kuwa usindikaji nyama ya binadamu unatokana na China kuishiwa nafasi ya kuzika maiti au kuwa Beijing inahifadhi nyama nyingine ambayo si ya binadamu kwaajili ya nchi zilizoendelea, na kuleta nyama ya binadamu nchi za Afrika.
----------------------------------------
PICHANI KUSHOTO: Moja ya maduka ya kuuza nyama katika soko Beijing
---------------------------------------
Huku uzushi huo ukizidi kusambaa, mtandao wa intanet wa Snopes.com umeweka picha zinazoonesha “miili ya watu” ikiwa ni picha za kutengeneza kutoka katika michezo ya video (video game) maarufu ya Resident Evil 6.

Pamoja na kulalamikiwa sana kwa tukio hilo katika vyombo vya habari nchini China, inaonesha kugusa hisia za Wachina wengi. Yang ametaka Zambia kufanya uchunguzi huku akidai Zambia imeomba radhi kupitia Naibu Waziri wa Ulinzi, Christopher Mulenga.


“Serikali ya Zambia imesikitishwa na tukio hilo licha ya kuwa na uhusiano mzuri kati ya China na Zambia” Mulenga alikaririwa na shirka la habari la Xinhua akisema na kuongeza “tutahakikisha idara husika za serikali zinafanya uchunguzi na kutoa taarifa kwa undani ya tukio hilo”

Nchi ya China ina uhusiano wa kibiashara na Zambia, huku serikali ya nchi hiyo ikifadhili miradi mbalimbali ya ujenzi na ikisaidia maliasili ya Zambia katika kukua kwa uchumi. Hata hivyo, uwepo wa China nchini Zambia umeleta hisia mbalimbali kwa wananchi wa Zambia, huku wakilalamikia wawekezaji wa China kulipa mishahara midogo na kufanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi. Kumeshakuwa na matukio mbalimbali yanayohusisha miradi ya China nchini Zambia, ikiwemo kulipuka kwa kiwanda mwaka 2005 na kusababisha vifo vya wafanyakazi zaidi ya 50.





No comments:

Post a Comment