Makamu wa Rais hahusiki na wala hajawahi kutoa agizo hilo. Ofisi inapenda kuujulisha umma wa Watanzania kuwa taarifa hizo ni za uzushi na zinapaswa kupuuzwa.
Tunatoa wito kwa Watanzania kuwafichua watu wa namna hiyo wenye tabia ya kutoa taarifa za uongo kwa kutumia jina la kiongozi huyu, huku vyombo vya serikali vikiendelea kuwasaka ili kuwajua na taratibu za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais anawasihi Watanzania kutumia muda mwingi kuchapa kazi ili kujipatia maendeleo kwenye maisha yao na siyo kutumia muda mwingi kufanya shughuli ambazo siyo za maendeleo kwa maisha yao binafsi.

No comments:
Post a Comment