Tuesday, February 09, 2016

WAFANYAKAZI AIRTEL WASHIRIKI KUKARABATI BUCHA KATIKA MPANGO AITEL FURSA

Morogoro Februari 7, 2016, Katika jitihada za kusaidia vijana wajasiriamali, wafanyakazi wa Airtel wameungana na shirika lao kupitia mpango wake wa Airtel FURSA kuwafikia vijana mkoani Morogoro. Mwishoni mwa wiki hii wafanyakazi hao walijitokeza kumsaidia kijana Hashim Mikidadi, kijana mjasiriamali anayejihusisha na kuuza bucha la nyama kwa kukarabati duka lake lililopo standi ya mabasi Ngerengere mjini Morogoro.

Akizungumza wakati wa zoezi la ukarabati wa bucha hilo Afisa mauzo wa Airtel, Aminata Keita alisema "Airtel tunajali sana jamii yetu inayotuzunguka hivyo tunaelewa changamoto nyingi ambazo vijana wamekuwa wakikutana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira, ukosefu wa mtaji wa kuanzisha biashara zao na mambo mengine mengi. Msaada wetu kama wafanyakazi wa Airtel ni kuunga mkono mpango wa kampuni yetu ya kusaidia vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel Fursa katika kusaidia vijana wetu kwa kuwaonyesha njia ili waweze kuinua jamii inayowazunguka na kufikia ndoto zao."
"Leo tunafuraha kubwa kuona kwamba tumeweza kumfikia na kumuwezesha kijana huyu mjasiriamali aliyewezeshwa na Airtel FURSA, ambaye Airtel Fursa imebadilisha maisha yake kwa kukarabati paa la bucha lake, kutengeneza sakafu kwa kuweka tiles za kisasa, na matengenezo mengine mengi ambayo imeipa duka hilo mtazamo mpya kabisa . Mapema wiki ijayo Airtel FURSA itamalizia kwa kumuwekea vifaa vya kisasa kabisa vikiwemo vifaa vya kukatia nyama, jokofu la kisasa la kuhifadhia nyama na vifaa vingine vnavyohitajika kwa kazi za bucha. Vifaa hivyo na gharama za utengenezaji vimegharimu kiasi cha sh. milioni 9, alisisitiza Aminata

Wakati wa shughuli hiyo ya makabidhiano, wafanyakazi wa Airtel walijiunga na wakazi wa Ngerengere ambao walijitokeza kumuunga mkono Hashim kwa kuwa na nidhamu kwa jamii inayomzunguka na ni mfano wa kuigwa na vijana wenzie.

Kwa upande wake Hashim aliwashukuru sana Airtel kwa kuweza kumpatia fursa hii kwani ni vijana wengi sana wanaohitaji msaada huu lakini leo hii nafasi hii imemdondokea yeye.

“Bila kuwasahau nawashukuru sana wafanyakazi wa Airtel kwa kusaidia ukarabati wa bucha langu kwani mtazamo huu mpya na vifaa vya kisasa utasaidia kuhamasisha wateja wangu na wale ambao hawakuwa wateja wangu.”.

“Nilianza nikiwa sina kitu. Lakini leo Airtel imeinua maisha yangu na kuniwezesha kuwapatia ajira vijana wenzangu waliokuwa mtaani bila kazi. ".

Airtel Fursa uwezeshaji ilizinduliwa mwezi Mei mwaka jana na ina tarehe kufikiwa vijana zaidi ya 3000 na mafunzo ya ujasiriamali na misaada ya biashara kwa karibu na 100 wajasiriamali bora vijana wote mmoja mmoja na katika vikundi vya vijana na hatimaye kukua kujenga fursa na jamii inayowazunguka. Katika msimu wa pili Airtel imeahidi kutumia zaidi ya sh. bilioni 1 katika mpango wa kuwawezesha vijana wa Tanzania kufikia uwezo wao katika ulimwengu wa biashara

Airtel Fursa awamu ya kwanza ulianza mwaka jana mwezi wa tano na mpaka sasa umeshaweza kufikia vijana zaidi ya 3000 kwa kuwapatia mafunzo ya biashara ya ujasiriamali na wengine wapatao 100 wameweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi vya kuendelezea biashara zao za ujasiriamali. Katika awamu ya pili Airtel Fursa imeahidi kutumia zaidi ya sh. bilioni 1 ukiwa na lengo la kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za biashara na vifaa vitakavyowawezesha kukuza biashara zao.

MWISHO

No comments:

Post a Comment