Thursday, February 04, 2016

MSICHANA MTANZANIA ALIYEPIGWA NA KUVULIWA NGUO KISHA KUTEMBEZWA MITAANI INDIA, AELEZA WAANDISHI YALIYOMKUTA

BENGALURU/New Delhi

Tukio la kusikitisha lilimtokea msichana mwenye miaka 21, Mtanzania saa moja na nusu jioni, Jumapili wakati akiwa na Watanzania wenzake watatu walipokuwa kwenye gari Ganapathinagar, nje kidogo ya barabara kubwa ya Hesaraghatta, Bengaluru, nchini India.

Ikiwa ni umbali wa kilometa 2 toka barabara kuu, nusa saa tu baada ya gari alilokuwa anaendesha mwanafunzi Msudani alipomgonga mwanamke aliyejulikana kama Shabana Taj, 35 na kupoteza maisha alipokuwa akitembea na mumewe Sanaullah ambaye ni fundi umeme.

Kundi la Wahindi waliochukizwa na tukio hilo walisimamisha gari alilokuwemo Watanzania hao.  Akieleza katika mahojiano kwa uchungu, bindi huyo alisema, “Tulitoka nje ya gari ambapo palikuwa na watu wengi wamezunguka gari. Pembeni alikuwepo polisi amesimama, nilimuuliza kimetokea nini, akajibu hakuna chochote. Rafiki yangu akanikimbilia na kuniambia nisisogee, wakati huo kundi hilo lilianza kumpiga” alieleza msichana huyo.

 “Wakanisukuma na kuanza kunipiga, nilikuwa nimevaa t-shet. Wakaivuta na kuichanachana, na kuniacha nikiwa mtupu. Wakaendelea kutudhalilisha tulipopata upenyo tukaanza kukimbia ili kuokoa maisha yetu.” Alihadithia Binti huyo.

“Nikiwa na wenzangu tuliingi kwenye basi, dereva hakuendesha badala yake abiria waliokuwemo wakatusukuma nje. Tukabakia mikononi mwa kundi hilo.” “ndipo msamaria mwema akanipa tshirt, ambapo na yeye akashambuliwa, waliendelea kutupiga mpaka tukaingia katika duka moja lililokuwa karibu” alisema

Wakati huo baadhi yao walishawasha moto gari letu na kuanza kulichoma na kuliteketeza. Wakati wanaelekea katika hospitali ya Sapthagiri, kundi hilo liliendelea kuwafukuza, hata walipofika hospitali kundi hilo lilidaiwa kutishia kuvamia hospitali hiyo kama Waafrika hawatatolewa nje.

Polisi imedai kuchukua maelezo ya msichana huyo jumatano, wakidhibitisha kupata maelezo hayo na kuchelewa kulichukulia hatua tukio hilo kwa siku tatu. Kiongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa kutoka Afrika, Bosco Kweesi amelaumu ajali ililosababishwa na Msudani hiyo na kusababisha kifo cha Shabana na kudai kuwa sheria ifuate mkondo.

Hata hivyo kushambulia watu kutokana na rangi yao ni jambo la kupinga kabisa, aliongeza kuwa suala hilo linafanyiwa kazi pia na balozi za nchi zote za Afrika wanazotoka wanafunzi hao.

Kweesi alisema, “ Mwanamke huyo amefariki na waliohusika na ajali hiyo wachukuliwe hatua. Lakini hawa waliodhalilishwa hawahusiki kabisa na tukio hilo”. Naye kiongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Tanzania alisema, walikimbilia kituo cha polisi jumapili usiku, kutaka msaada ili wawapeleke wenzao hospitali.

Alisema “ Polisi waligoma kutusaidia na hata kusikiliza malalmiko yetu, wakati huo polisi walikuwa wanamshikilia mwenzetu ambaye hausiani kabisa na tukio hilo. Polisi mmoja akatuambia kuwa nyie wote mnafanana na mwezenu ataachiwa mkimleta dereva aliyesabababisha” alieleza.

“Sasa hivi tunamuogopa kila Muhindi anayetusogelea, baada ya yaliyonikuta”, aliongea msichana huyo Mtanzania mwenye umri wa miaka 21 anayesoma City College wakati akiongea na waandishi wa habari katika hospitali ya Sapthagiri, ambapo alipelekwa kwaajili ya vipimo mbalimbali.

Waziri wa Uhusiano wa Mambo(External Affairs Minister) ya Nje Sushma Swaraj, akionesha kuwa na taarifa aliweka katika mtandao wa twitter akisema “Tumeumizwa sana juu ya tukio la aibu alilofanyiwa msichana wa Kitanzania huko Bengaluru”

Waziri huyo ameitaka serikali kuhakikisha usalama na ulinzi kwa wanafunzi wote ambao ni wageni nchini humo. Katika taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania nchini India ilimtaka Waziri Sushma Swaraj kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wale waliomdhalilisha msichana huyo.

Jumatano iliyopita Polisi wa Bengaluru walifungua kesi chini ya kifungu 354 IPC dhidi ya watu ambao hawakufahamika, wakati ambapo watu wanne walikamatwa jioni siku hiyo.




No comments:

Post a Comment