Sunday, January 24, 2016

MASHINDANO YA MICHEZO YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU YAFUNGULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Leonard Tadeo akikabidhi Jezi kwa moja ya timu zinazoshiriki katika mashindano ya michezo yanayohusisha wanafunzi wa vyuo vikuu leo jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia kwake ni mwenyekiti wa shirikisho la vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam Bw.Imani Matabula.
 
Mwenyekiti wa shirikisho la vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam Bw.Imani Matabula(aliyesimama) akimkaribisha Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Leonard Tadeo(kushoto) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya michezo vya chuo kikuu cha Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Leonard Tadeo akikagua timu ya chuo kikuu cha Dar es salaam wanaokaa Chuoni wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya michezo vya chuo kikuu cha Dar es Salaam.
















No comments:

Post a Comment