Ikiwa ni siku ya tano tangu Washiriki 20
wa Shindano la Bongo Style linalo andaliwa na asasi isiyo ya Kiserikali ya Faru
Arts and Sport Development Organization (FASDO), ikiwahusisha Wapiga picha na
wabunifu wa mavazi wenye umri kati 19-25 walioingia rasmi kambini Novemba 5
mwaka huu,ambapo washiriki hao wameendelea kujifua zaidi huku wakipewa kazi
mbalimbali za ubunifu na masomo mengine ikiwa ni sehemu ya shindano hilo.
Wakiwa kambini washiriki hao
wamepata nafasi ya kujifunza mambo mapya ambayo walikuwa hawayafahamu. Fainali
hizi zinatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu ndani ya ukumbi waAlliance
Francaise Jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa
upande wa picha wamekili kuwa walikuwa wanaona kama wanafahamu vema kupiga picha
lakini baada ya kupata somo wamegundua kuwa kuna mambo mengi ambayo walikuwa
hawayafahamu na menginewalikuwa wanayafanya lakini bila kujua kuwa walikuwa
sahihi.
Pia waliongeza kuwa
wanashukuru kuwapata wataalam ambao wameweza kuwaonesha ni jinsi gani
wanatakiwa kuwa wapiga picha wazuri.
Nao washiriki wa
ubunifu wa mavazi wameshukuru kupata wataalam ambao wamekuwa wakiwapa maelekezo
mengi ambayo yalikuwa ni chachu kwao kwasababu kila mmoja kwa upande
wake wamejifunza mambo mapya mengi na kuona kuwa kumbe sio lazima kuwa na ubunifu
wa aina moja ya mavazi lakini wanaweza wakawa na aina nyengine nyingi kulingana
na mazingira waliyopo na kuishukuru Fasdo kwa kuwakutanisha.
Mwalimu na mtaalam wa kupiga picha Sameer Kermalli amekili kuwa tangu darasa
lianze washiriki hao wamekuwa na uelewa wa haraka na yeye kupata nafasi ya kuwaelekeza
mbinu mbalimbali za kupiga picha na kanuni mbambali za upigaji picha, washiriki
hao wamekuwa wasikivu na wameongeza ubunifu zaidi jambo ambalo limemtia moyo
mtaalam huyo.
Kwa upande wa Mbunifu wa mavazi Martin kadinda(pichani juu) alisema kuwa washiriki wapo vizuri na kila mbunifu anakitu chake cha kipekee ambacho yeye anafanya mfano wapo wale ambao wanabuni nguo zao kwa kutumia kitenge tu, wengine wanatumia vitu vya asili, nguo za kisasa, nguo ambazo zipo tayari kwa ajili ya kuvaliwa na zenginezo, aliwashauri kuwa wasiegemee katika kitu kimoja tuu au aina moja ya mavazi lakini wawe na ubunifu na kubadilika kila wakati kwa sababu mitindo inakwenda ikibadirika.
Mkurugenzi Mtendaji wa
FASDO, Tedvan Chande alipata nafasi ya kutembelea kambini na kujionea jinsi
washiriki wanavyojituma katika kazi zao na maandalizi ya shindano hilo yanavyo
kwenda.
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande akiwa na washiriki wa shindano la Bongo Style ambao hawapo pichani , akiwa na Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alipofika kuwatembelea na kuongea nao machache.
Baadhi ya Washiriki kwa upande wa Ubunifu wa mavazi wakiwa wanachakalika kuandaa kazi zao mbalimbali
washiriki wa ubunifu wa mavazi wakiendelea na kazi
Tunukiwa Daudi (Aliyesimama) akitoa somo juu ya matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na Faida zake.
Baadhi ya washiriki upande wa kupiga picha wakifurahia jambo.
Muwezeshaji kutoka Wiki Loves Africa akitoa somo juu ya upigaji picha kwa washiriki ambao hawapo pichani.
Hawa ni washiriki kwa upande wa kupiga picha wakikamilisha moja ya mazoezi waliyopewa(Picha kwa hisani ya Washiriki upande wa wapiga picha).
No comments:
Post a Comment