Saturday, December 20, 2014

SHABIKI WA MAN U AMNG’ATA NA KUMNYOFOA SIKIO SHABIKI WA ARSENAL

Shabiki wa Asernal amepoteza sehemu ya sikio lake usiku wa jumamosi iliyopita baada ya kutambiana na mwenzie ambaye ni shabiki wa Manchester United kufuatia mechi kati ya timu hizo za Ulaya.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, kijana (PICHANI KUSHOTO) mwenye umri wa miaka 16, mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari ya wavulana, Kisumu Boys High School ameng’atwa sikio lake la kulia na kunyofolewa kipande na mvulana mwingine ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili.

Katika mechi ya siku hiyo United ilishinda 2-1 dhidi ya Arsenal. Akieleza kijana huyo alidai kukutana na rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Kato akiwa anaelekea nyumbani wote wakitoka kuangalia mechi hiyo iliyokuwa inaoneshwa katika televisheni katika kumbi mbili tofauti.


Inadaiwa Kato alimuanza kwa kumwambia asingepoteza hela zake kwenye mechi ile kumuangalia “mama” anavyofungwa. Akichukizwa na kauli hiyo, akampiga Kato usoni. Kato akaondoka kama vile yamekwisha.

“baada ya hatua chache, akanifuata… akanishika begani, sikujua kama alitaka kuning’ata.

“ghafla akakamata sikio langu kwa meno yake. Mpaka alipong’ata na knyofoa kipande cha sikio langu na kulitema chini, akatokomea gizani” alisema kijana huyo. Ambaye alipata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kisumu Mashariki









No comments:

Post a Comment