Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wa Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio
wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (Chawaumavita), Hillar Said
(kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo , kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Watu, Watoto wenye
mtindio wa ubongo yatakayofanyika, Oktoba 7, 2015 viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa chama hicho, Mwanahamisi
Hussein.
Katibu wa chama hicho, Mwanahamisi Hussein (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Baadhi ya Waandidhi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano huo wakifuatilia kwa karibu.
CHAMA cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa
Ubongo, Akili na Viungo (Chawaumavita) kimewataka wanaume kuacha
tabia ya uoga ya kukimbia majukumu pindi wanapopata watoto wenyeulemavu.
Katika hatua nyingine chama hicho kimewaomba wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa kuzungumzia namna watakavyoweza kuwasaidia
walemavu katika mikutano yao.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Watu na WatotoWenye Mtindio wa Ubongo ambayo huazimishwa kila mwaka ifikapo Oktoba 7. Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Hilal Saidi, alisema watoto wenye matatizo hayo wanapaswa
kusaidia badala ya kuwatenga.
Amesema kuwa katika tafiti walizofanya wamegundua kuwa wanaume wengi ni waoga wa majukumu pindi wanapopata watoto
wenye ulemavu hadi kupelekea kukimbia familia zao.
"Wanaume wengi waoga wa majukumu hasa anapozaliwa mtoto mwenye ulemavu, wanaona kuwa ni mkosi mkubwa na kuanza kupata msukumo katika familia yake kuachana na mkewe hivyo anateleleza familia
huku mwanamke akibaki peke yake" anasema Said.
Hata hivyo alisema ulemavu umegawanyika katika makundi matatu ambayo ni ulemavu wa akili,mtindio wa
ubongo na viungo,alisema watoto wenye ulemavu wa viungo na mtindio wa ubongo wanaweza kupatiwa matibabu hali yao ikawa sawa na ushiriki
katika katika elimu na kufikia malengo yao.
Hivyo amewataka wakina baba na familia kwa ujumla kutowafungia ndani watu wenye ulemavu na badala yake kuwapeleka
katika vituo vya afya kwaajili ya matibabu na miili yao
ikatengemaa.
No comments:
Post a Comment