Monday, August 24, 2015

WALIOTAKA KUOLEWA NA AL-SHABAAB WATIWA MBARONI

Wanawake wawili raia wa Kenya na Tanzania pamoja na watoto wao watatu wanashikiliwa na Polisi nchini Kenya, baada ya kukamatwa Mjini Garissa wakiwa katika jitihada za kujaribu kutorokea Somalia kujiunga na Al-Shabaab kwa minajili ya kuolewa.

Mabibi harusi hao watarajiwa Bi. Fatuma Bariki Makame (28) kutoka Tanzania na Bi. Swabra Abdallah (23) wa Kenya, walivurugwa na kundi hilo kupitia mtandao wa intaneti kwa ahadi za kupata neema ya kuolewa na wapiganaji wa kundi hilo.

Walikamatwa wakisafiri na watoto wao watatu wenye umri wa miaka Saba, Minne na miwili.
Taarifa ya kiusalama imesema kukamatwa kwao ni sehemu ya uchunguzi wa Polisi unaoendelea wa mtandao wa A-Shabaab, wanaolenga kuchukua vijana wa kike na wakiume, kwa kuwa matukio ya kutoweka kwa vijana wa kiume na kike nchini Kenya yamekuwa yakijitokeza kwa wingi.
SOMA ZAIDI.....


Pamoja na hilo wazazi wa vijana nchini humo wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na mamlaka za kiusalama, kwa kutoa taarifa za vijana wote ambao huenda wamesafiri kuelekea Somalia kujiunga na Al-Shabaab.

Kukamatwa kwa wanawake hao huko Garissa kumetokea ikiwa ni wiki moja baada ya taarifa nyingine ya serikali, kuonyesha takriban shule sita ziko chini uangalizi wa kiusalama kutokana na idadi ya wanafunzi wanaoacha shule kujiunga na makundi ya kigaidi ya Somalia na Syria.


No comments:

Post a Comment