Monday, August 24, 2015

RAY C KUANDAA DOCUMENTARY YA MAISHA YAKE

Mwanamuziki nchini Tanzania, Rehema Chalamila ‘Ray C’, (Pichani kushoto) amefunguka na kudai kuwa amekuwa kimya kwa muda kutokana na kuandaa makala ‘Documentary’ kuhusu maisha yake aliyoyapitia ya utumiaji wa dawa za kulevya.

Amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa amepata wahisani kutoka nchini Ujerumani, na kuweza kuisaidia Ray C Foundation, kuweza kuandaa makala hiyo ambayo itaonesha maisha yake ya muziki na jinsi alivyoanza kutumia dawa hizo za kulevya na mambo mengine.

Kupitia mtandao wa kijamii ameandika “Sitakiwi kuongea ila kwa sababu Documentary inakamilika muda si mrefu nimeona niwambie tu kuwa Ray C Foundation imepata Donor mkubwa sana kutoka Germany.na tayari tumeshaanza kushoot Documentary ya maisha yangu ya Uteja!

Documentary hii inanihisu Mimi kama mwanamuziki itaonyesha jinsi gani nilivyoanza kuvuta madawa ya kulevya na majanga yote niliyofanya ili niweze kununua unga na mengi sana mabaya niliyokutana nao kipindi niko hoi na unga”

No comments:

Post a Comment