Monday, June 01, 2015

BREAKING NEWS: KIM NA KANYE KUPATA MTOTO WA PILI

Kim Kardashian West na Kanye West wanategemea kupata mtoto mwingine ikiwa ni miezi 23 toka wapate mtoto wao wa kwanza wa kike aitwaye North. Taarifa hizo zilitolewa katika kibwagizo cha tamthiliya ya Keeping Up with Kardashians, jana jumapili.

Mtandao wa jarida la Time uiliripoti kuwa tamthiliya hiyo inayooneshwa katika chanel ya E!. Chaneli hiyo ilitoa pongezi zake kwa Kim kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa twitter ‘Congratulations Kardashian, (34)’ baada ya taarifa hiyo.
Star huyo wa show ya televisheni inayoonesha maisha yake alisi ya kila siku, amenukuliwa mara kadhaa akilalamikia changamoto za kuongeza familia yake. Kim alisikika akimwambia nduguye Kendall Jenner katika kipindi hicho mwezi wa nne kuwa “ Nimekuwa nikilalamika mara nyingi tu jinsi nnavyochukia kuwa mjamzito, sikutegemea kuomba kubeba ujauzito mara nyingine”

BOFYA KUSOMA ZAIDI...

“Kupata mtoto wa pili sio faraja kama ilivyokuwa kwa mtoto wa kwanza…ni kama nna kwenda hedhi dakika tano zijazo”
Vyanzo vimeeleza kuwa Kanye (37) amesema anasubiri mtoto wa pili, jambo ambalo limebadilisha maisha yake toka kuzaliwa kwa North.
Alieleza Gunnar Peterson, “ watu wengi wana wasiwasi kuwa baba kunaweza kumnyang’anya kazi yake au hata kuvunja mahusiano na mke wake, lakini mambo yameendelea kuwa mazuri kwa Kanye tokea amekuwa baba”
Wakati Kanye na Kim wanasherehekea mwaka mmoja wa ndoa yao, furaha hiyo imeongezeka baada ya Kim kupata ujauzito wa mtoto wa pili.
“Kim na Kanye wanafurahia kuwa wazazi” chanzo kilichoko karibu na Kardashian kililiambia jarida la PEOPLE “na wanapenda sana kutumia muda mwingi nyumbani wakiwa kama familia” (Time)


No comments:

Post a Comment