Tuesday, March 17, 2015

HAKUTAKUWA NA TAIFA LA PALESTINA NIKIWA WAZIRI MKUU…NETANYAHU

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (Kulia), amesema hataruhusu kuundwa kwa taifa la Palestina akiwa madarakani, matamshi ambayo ameyatoa katika mkesha wa uchaguzi mkuu nchini Israel.

Kauli zake katika mtandao wa Israeli ni jaribio la kutaka kuungwa mkono kwa chama chake cha Likud, kulingana na kura ya maoni inayoonyesha kuwa wapiga kura nchini humo bado hawajaamua nani wampigie kura.

Kura hiyo ya maoni inakiweka chama cha Likud nyuma kidogo ya chama cha Zionist Union, chenye mrengo wa kati kushoto na mabcho kimesema kitarejesha uhusiano na Wapalestina na jumuia ya kimataifa kikiingia madarakani.
Kwa upande wake kiongozi mwenza wa Bwana Netanyahu, Yitzhak Herzog, amesema ataiunganisha nchi baada ya kipindi kirefu cha mgawanyiko.

Uchaguzi mkuu wa Israel unafanyika leo.(BBC)

No comments:

Post a Comment