Friday, October 10, 2014

BREAKING NEWS: BARABARA ZIMEFUNGWA, JIJINI DAR ES SALAAM (ANGALIA HAPA)

Kampuni ya watengenezaji barabara STRABAG inayotengeneza mtandao wa barabara za mabasi ya mwendo kasi BRT, pamoja na wadau wengine imetoa matangazo leo tarehe 10/10/2014 katika vyombo vya habari yanayo onesha kufungwa kwa barabara ya Kinondoni na matumizi ya Barabara ya Kawawa na Morogoro.

Katika matangazo hayo mawili, STRABAG, imetoa michoro inayoonesha jinsi njia mbadala zitakavyofanya kazi ili kuhakikisha shughuli na matumizi ya barabara yanaendelea.

Kwa wale wanaotumia Barabara ya Kawawa kutokea Kinondoni Morocco kuelekea Magomeni wametakiwa kufuata maelekezo kama mchoro unavyoonesha.

STRABAG pamoja na wadau wenging wa pia wametoa marekebisho ya matumizi ya makutano ya barabara ya Morogoro na Kawawa na kwamba matengenezo katika kipande hicho yataanza tarehe 10 na kukamilika 25 Oktoba, 2014





No comments:

Post a Comment