Tuesday, October 07, 2014

ANGALIA AKON ALIVYOJIKINGA NA VIRUSI VYA EBOLA ALIPOKUWA DR-CONGO

Akiwa katika ziara nchini DRC katika kongamano la kimataifa la amani lijulikanalo kama International Day of Peace huko Goma, Akon alipokelewa na umati mkubwa wa watu akiwa katika tufe lililo mfano wa bubble (pichani juu).

Goma ni mkoa ulioko mashariki ya DRC (Democratic Republic of Congo) eneo ambalo limekuwa na matatizo ya amani nchini humo huku likitekwa mara kadhaa na waasi wa Kongo. Akon alilakiwa na kundi la watu wasiopungua 60,000.

Kwa mujibu wa mtandao wa nchini Marekani wa Vibe, waendesha mitandao ya jamii waliingia mitandaoni na kuanza kuzungusha uvumi kuwa Akon aliletwa katika tufe hilo kwa lengo la kukwepa kuambukizwa virusi vya EBOLA.

Kwa mujibu wa Noisey, msanii huyo hakufanya kitendo hicho kwa lengo la kukwepa maambukizi ya EBOLA, na imeripotiwa mara kadhaa kuwa Akon ameshawahi kufanya matamasha kadhaa kwa mtindo huo wa kuletwa katika tufe ikiwa ni pamoja na Austranila na Dubai.

No comments:

Post a Comment