Taarifa zilizotufikia zimesema kuwa kivuko hicho (Mv Dar es Salaam) kilichookuwa kinajengwa na kampuni ya nchini Denmark kimeshuka leo majini tayari kuanza safari ya kuja dar es salaam na kutarajiwa kuingia jijini DSM ndani ya wiki tatu mpaka nne.
Kivuko hicho kitakuwa na kasi kuliko kivuko chochote katika Bahari ya Hindi hususani katika pwani ya Afrika Mashariki ukiacha Afrika Kusini.
Kivuko hichi ni mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Ujenzi katika kupunguza msongamano katika barabara za jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment