Wednesday, June 18, 2014

YANGA YAJIPANGA KINIDHAMU ZAIDI, ATAKAYE TIBUA OUT

Klabu ya Yanga ya jiji Dar es Salaam imetangaza mpango wa kuwafuta uanachama wa klabu yao wanaoenda kinyume na kanuni za Yanga.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana Dar es Salaam Mwenyekiti wa matawi wa kilabu hiyo ya Yanga Mohamed Msumbi alisema kuwa yeye na kama kiongozi anapingana na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo wasio itakia mema timu yao.

"Napingana na wanachama waliopeleka barua Shirikisho la Soka nchini (TFF, kwa lengo la kupinga maamuzi ya wanachama walio pendekeza kumuongezea muda wa mwaka mmoja Rais wa Klabu hiyo Yusuf Manji na hivyo wanachama hao watafutiwa utambulisho wao ,"alisema.
Msumbi alisema kuwa wanachama hao , watafutiwa uanachama wao kutokana na kwenda kinyume na katiba ya Yanga.
Kiongozi huyo alibainisha kuwa katika katiba ya Yanga Ibara ya 10 inayo husu haki za wanachama inamaelezo yanayomtaka mwanachama hai wa Yanga namna anavyotakiwa kuwa ambapo kipengele cha kwanza kinasema mwanachama anahaki ya kujua ajenda ya mkutano mkuu wowote na kuitwa mkutanoni katika muda uliotajwa ,kushiriki katika mkutano,kufanya uamuzi kuhusumasuala ya Yanaga na kutumia haki yao ya kupiga kura.
Mwenyekiti huyo alitaja kipengele kingine cha sita kinacho zungumzia haki ya kujitetea au kutoa maelezo yake mbele ya kikao cha klabu kinchohusika katika mashtaka yoyote yaliyotolewa juu yake , pamoja na haki ya kukata rufani ya kwenda katika kikao cha juu cha klabu,kamakipo endapo hakuridhika na uamuzi uliotolewa.
Msumbi alisema kuwa alisema kuwa moja ya haki nyingine katika katika ibara hiyo ya haki za mwanachama wa klabu ya Yanga ni moja wapo ni kipengele cha saba kinacheelezea haki ya mwanachama ya kumuona kiongozi yeyote wa klabu mradi tu awe amefuata utaratibuuliowekwa.
Kiongozi hiyo wa matawi wa Yanga aliweka wazi kipengele kingine cha mwisho ambacho ni cha nane kinachoeleza kuwa haki ya nyingine zote zinazotokana na Sheria hizo au zile zinazo tambuliwa na kanuni , maagizo na maamuzi ya DRFA na TFF.

Msumbi alisema kuwa vyanzo vya migogoro kama ya wanachama hao waliotajwa kufutwa uanachama wao ; migogoro kama hiyo ndani ya klabu inafanya klabu kutotekeleza malengo na hivyo kusababisha kushinda kupatikana kwa maendeleo ndani ya klabu.
Pia alisema wao wanaamini mpinzani wao ni timu ya Simba ya Dar es Salaam ambapo klabu mpya ya Azam ni maadui zao kwani katika migogoro kama hiyo wao wanaweza kufaidika .



No comments:

Post a Comment