Wednesday, June 11, 2014

TFF YAMREJESHA RASMI WAMBURA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS

Rasmi Kamati ya Rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemrejesha Mgombea wa Urais wa Simba Michael Richard Wambura kwenye mbio za kuwania uongozi wa Wekundu wa Msimbazi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Julius Lugaziya amewaambia Waandishi wa Habari mchana wa leo ofisi za TFF katikati ya Jiji la Dar es Salaam, kwamba Wambura amerejeshwa baada ya kikao chao kilichodumu kwa siku mbili.
Baaada ya mgogoro mrefu tangu juzi Saa 5:00 asubuhi hoteli ya Courtyad, Upanga, Dar es Salaam hadi jioni ya jana, Wajumbe wa Kamati hiyo waliamua kupiga kura kuamua na Wambura akapata kura tatu kati ya tano za kumkubalia aendelee na mbio za Urais Simba.
Na mambo yalio mfaya aweze kurudi rasmi katika kinyang'anyiro hicho ni sababu japokuwa samba walimsimamisha asiwr mwanachama wa klabu hiyoo bado walikuwa wakimshirikisha katika vikao vyo vya maadili pia wambura hadi sasa ni mjumbe wa kamati ya samba kwa vipengele hivyo inaonesha kabisa wambura halali kuendelea kugombea nafasi ya uraisi.
Ikumbukwe Wambura alikata rufaa TFF akipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kumuengua katika kinyang’anyiro cha kuwania urais katika uchaguzi wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Kamati ya Uchaguzi ya Simba chini ya Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro ilimuengua Wambura kwa sababu alikiuka Katiba ya klabu hiyo, TFF na FIFA kwa kuipeleka klabu hiyo mahakamani.
Wambura sasa atachuana na Evans Aveva, mgombe anayeoongoza kuungwa mkono katika mbio hizo.


No comments:

Post a Comment