Sunday, June 01, 2014

TAHADHARI PICHA INATISHA: MAJAMBAZI YAUA MTU ARUSHA SASA HIVI

PICHA: Mtu mmoja amepigwa risasi zisizojulikana idadi yake na kupoteza maisha katika eneo la Clock Tower Jijini Arusha na majambazi waliotoka kupora fedha katika duka la kubadilishia fedha la Northern Beureau, muda mchache uliopita.

Taarifa zilizotufikia dakika chache ziliopita ni kwamba majambazi yamevamia na kupora fedha katika duka la kubadilishia fedha jijini Arusha ikiwa ni dakika chache zilizopita tokea sasa. Duka hilo la fedha linalojulikana kama Northen Bureau de Change, liko katikati ya jiji hilo katika eneo la Mnara wa Saa (Clock Tower)

Bofya soma zaidi kwa picha zaidi...

Katika tukio hilo mtu mmoja aliyekuwa anapita njia akaona tukio hilo akaamua kupiga kelele za wezi ndipo aliponyamazishwa kwa maisha yake yote kwa kupigwa risasi nyingi na kufa hapohapo.




No comments:

Post a Comment