Wednesday, June 18, 2014

NEWS ALERT: MTOTO WA AJABU AZALIWA NCHINI

VIA JUSTINA GEORGE: Mtoto wa ajabu amezaliwa huko wilayani Makete mkoani Njombe usiku wa kuamkia tarehe kumi na saba june 2014.Ukimuona mtoto ngozi yake ni kama amevaa koti kubwa kushinda uwezo wa mwili wake akiongea na blog hii reporter Daima kyando alisema mtoto huyo wa ajabu alikua na tumbo kubwa lililomeza viungo vingine vya mwili kama miguu,mikono,kiuno na shingo.Akiendelea zaidi reporter huyo mahiri alisema mama wa mtoto huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja alikua na afya nzuri na kuonesha kuwa mimba yake ilikua ya kawaida kwani alihudhuria clinic kama kawaida na hakupatikana na matatizo yoyote.

Habari zaidi zinasema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa amekwisha fariki na alizaliwa kwa njia ya upasuaji,chanzo cha tatizo la mtoto huyo hakikuweza kufahamika mara moja mpaka tunaenda mtandaoni madaktari walikuw wakiendelea na uchunguzi.






No comments:

Post a Comment