Saturday, May 17, 2014

MWALIMU NYERERE AMTOKEA MKEWE, SOMA ALICHOMWAMBIA KUHUSU NCHI

Mjane wa aliyekuwa Rais wa kwanza na muasisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere(PICHANI JUU) kwa mara ya kwanza toka mumewe afariki, ametoka na kuongea mbele ya waandishi wa habari kuhusu hatma ya nchi ya Tanzania.

Akiongea na waandishi nyumbani kwake Msasani, jana, Mama Maria alisema kwa uchungu kuwa mumewe ambaye alifariki miaka 15 iliyopita, amemtokea na kumtaka akalitahadharishe taifa na mwenendo wake.


“Kitendo cha nchi kukumbwa na mashetani wanaovuruga amani na kutukana waasisi kimenfanya Mwalimu Nyerere kunitokea na kunitaka kuliambia taifa kusali na kuomba sana kwani nchi inaelekea katika vita” Alisema jana huku akionesha hisia kali.

Mama Maria aliongea kwa uchungu na hata maafisa wa usalama walipojaribu kumfupisha alikataa na kusema “wacha niseme leo.” Tanzania ilingia katika mchakato wa kutafuta katiba mpya, ambao ulipata baraka zote za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mpaka kufikia hatua ya Bunge Maalumu la Katiba.

Bunge hilo lilikutana kwa muda wa siku 70 na kuleta mvutano mkali ambao ulisababisha kutotimiza lengo la kupata katiba mpya. Wabunge walitakiwa kujadili rasimu ya katiba iliyoletwa baada ya kukusanya maoni kutoka kwa Watanzania kupitia Tume ya Maoni ya Katiba iliyoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba.

Katika bunge hilo walisikika baadhi ya wajumbe waliounda kundi la UKAWA(Umoja wa Katiba ya Wananchi) wakitoa maneno yaliyowakejeli waasisi wa Taifa la Tanzania ambao ni Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanganyika, pamoja na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.

Mama Maria aliwaambia waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari jana kuwa na kuwatahadharisha Watanzania kutodhubutu kuwapa nchi watoto wasio na lishe bora kuanzia kwa mama. Akiashiria kutokuwa na busara ya kushika na kuliongoza taifa la Tanzania.

Hata hivyo Bunge Maalumu la Katiba lilishindwa kufikia muafaka baada ya kundi la UKAWA kutoka nje kutokana na matumizi lugha zisizofaa na kuleta hasira na chuki ndani ya bunge hilo na kuwaacha kundi la Tanzania Kwanza ambalo idadi yake kubwa ni wajumbe wa chama tawala cha CCM, wakiendelaa na mijadala huku wakiwataka UKAWA kurudi ndani ya Bunge ili kuendelea na mijadala.

Mwenyekiti wa Bunge Hilo, Samweli Sitta aliliahirisha bunge hilo mpaka agosti tano mwaka huu, kwaajili ya kupisha bunge la Katiba kuendelea na ratiba zake, kwa matumaini ya kupatikana kwa katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1 comment: