Friday, May 16, 2014

KOREA KASKAZINI WAMWITA OBAMA NYANI, AENDE KWENYE PORINI AFRIKA

Ikulu ya Marekani, White House, imekosoa ubaguzi wa rangi dhidi ya Rais Obama katika taarifa iliyotolewa na kiongozi wa taifa la Korea Kaskazini. Viongozi wa Ikulu wamekuja juu kuhusu hotuba iliyomtaja Obama kuwa “mtu mchafu (dirty Fellow)” asiyekuwa hata na muonekano wa kawaida wa binadamu” liliandika gazeti la Washington Post.

Chapisho hilo dhidi ya Rais Obama liliandika “Itakuwa vizuri Obama angeishi na kundi la nyani katika zoo kubwa kuliko zote duniani na kulamba mikate inayorushwa na watembelea zoo”

Kujibu maneno hayo machafu, Ikulu ya White House iliita Pyongyang “haswa kuwa ni wabaya na wasio na heshima.” Kwa kawaida White House huwa inadharau matusi toka Korea Kaskazini, lakini hii ilikuwa ni ya kudhalilisha sana kiasi kwamba White House ilidhamiria kujibu.

“Wakati serikali ya Korea ya Kaskazini ndio inayodhibiti vyombo vya habari, pamoja na maigizo yenye kutia chumvi, haya maneno ni mabaya na yasiyo na heshma” alisema Caitlin Hayden, msemaji wa National Security Council, katika taarifa, kwa mujibu wa gazeti la Washington Post.
Vyombo vya habari vya Korea ya Kaskazini, vinavyodhibitiwa vinafahamika kwa kutokuwa na subira, lakini havikuwahi hata siku moja kumshambulia rais wa Marekani kwa namna binafsi nay a kudhalilisha namna hiyo.
Obama ana “damu ya mchanganyiko” nab ado anafananishwa na nyani wakati jamii ya mwanadamu imebadilika kwa zaidi ya mamilioni ya miaka, liliandika gazeti la Korea ya Kaskazini.
Taarifa hiyo iligunduliwa na Joshua Stanto, ambaye mara nyingi huwa anaposti taarifa Korea Kaskazini zinazohusiana na uvunjifu wa haki za binadamu. Pia aligundua posti nyingine iliyoonesha kuwa Obama ni nyani wa ajabu.

SHUKA CHINI UWEKE MAONI YAKO TAFADHALI. . .


No comments:

Post a Comment