Angalia kipande cha video kinachosambaa sasa hivi kwenye
mitandao kinachomuonesha mtu aliyepigwa na kuangushwa na kitu kisichojulikana
na wala hakionekani zaidi ya kivuli. Tukio hilo lilinaswa na kamera za CCTV
katika corridor ambapo mtu aliyejifunika kichwani kwa kutumia hood alipokumbwa na mkasa huo.
Picha hiyo haina sauti, inaelekea ni kamera ya ulinzi ndio
ilikamata tukio hilo, kwani kamera hiyo inaonesha haina microphone kwaajili ya
kunasa sauti.
Video hiyo inaonesha mtu huyo alipofika mwisho wa korido
kivuli kisichokuwa na sura kilitokea kusikojulikana kinaonekana. Jamaa na
kujiamini kwake kote ghafla kulionekana kupotea baada ya kuvamiwa na kudondoshwa
chini, kabla ya kufanya lolote alishikwa mguu na kuanza kuburuzwa huku akiwa
mgongo chini.
(ANGALIA VIDEO LIVE UONE, BOFYA CHINI)
Mwathirika huyo wa janga la mzimu, ambaye hakuweza
kutambuliwa, lazma alihisi siku zake ndio zimefikia mwisho, aliinuka upesi na
kutimua mbio kuelekea alikotokea.
TAFADHALI SHUKA CHINI UTOE MAONI YAKO. . .
No comments:
Post a Comment