Msanii wa Bongo Movie nchini, Irene Uwoya(Kushoto) amezua amesababisha mahusiano ya Msami Giovani(Kulia), ambaye ni mwalimu wa muziki kuvunjika na kumfanya aliyekuwa mpenzi wa mwalimu huyo kufunguka kuhusiana na suala hilo.
Uwoya ambaye kwa sasa katekwa na kuzama katika penzi la chipukizi huyo anayefundisha kucheza muziki kutoka katika nyumba ya vipaji (THT) amsababisha aliyekuwa mpenzi wa Msami, Rehema kuweka hadharani sababu za mahusiano yake kuvunjika.
Rehema aliweka wazi alipohojiwa na blog ya Immamatukio jana, ambapo mwandishi alipokutana naye Sinza, katika mizunguko yake. Akizungumza na kwa uchungu kuhusu aliyekuwa mpenzi wake, Rehema alisema Irene alitumia msuli wa pesa kumteka mpenzi wake kimahaba.
“Irene ndio alimtokea Msami, na wala hakujali kama Msami anamahusiano” alisema Rehema na kueleza kuwa njaa ndio iliyompeleka Giovani kwa Irene.
“Kilichomfanya Msami akubali kuwa “Serengeti boy” wa Uwoya ni sababu amekuwa akiwezeshwa kifedha ambazo ndo zinamweka mjini,” alieleza Rehema na kuendelea kuwa Msami yuko na Uwoya sababu ya tamaa tu ya kuwa na maisha mazuri na si vinginevyo.
Hata hivyo alipoulizwa kama bado anampenda Msami, Rehema alijibu “nampenda sana tu maana tumetoka mbali na tumekuwa pamoja mda muda mrefu sana.” Jitihada bado zinafanywa kumpata Msami Giovani ili kueleza kuhusu ukweli wa alichokisema Rehema.
No comments:
Post a Comment