Thursday, May 29, 2014

BILIONEA WA MANCHESTER UNITED AMEFARIKI

Bilionea Malcolm Glazer(kushoto), aliyeshinda tenda ya utata ya kuichukua Manchester United mwaka 2005, amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 85. Mfanyabiashara huyo wa Marekani atakumbukwa kama bilionea wa Florida aliyeichukua kuimiliki binafsi Man U miaka tisa iliyopita na kuwekeza zaidi ya pauni milioni 500 za Uingereza.

Glazer amekuwa mgonjwa kwa muda sasa na kuwaachia shughuli za uendeshaji wa United watoto wake wa kiume, Joel na Avram. Msemaji wa United amesema: "Fikra za kila mmoja katika United zipo kwa familia usiku huu,"

Familia ya Glazer bado wanamiliki Tampa Bay Buccaneers, timu ya mpira wa miguu ya Marekani waliyoinunua mwaka 1995. Na kwenye tovuti ya Bucs, ambako zimetangazwa habari za kifo cha Glazer.

Wakati wa umiliki wa Glazer, United imeweza kushinda mataji matano ya Ligi Kuu ya England na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Glazer ameacha mke, Linda waliyefunga naye ndoa mwaka 1961 na watoto sita, Avram, Kevin, Bryan, Joel, Darcie na Edward.

No comments:

Post a Comment