Friday, April 18, 2014

UKAWA YAPANIA KUZUNGUKA NCHI NZIMA, KUELEZA WANANCHI

Dodoma.

Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaunda Umoja  wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wamepanga kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima ili kuongea na wananchi juu ya msimano wao wa kususia Bunge hilo.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini hapa Mwakilishi wa kundi hilo Profesa Ibrahim Lipumba alisema kuwa katika kikao chao wamekubaliana kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara kwa wananchi ambapo wataanza mkutano huo kesho kutwa Jumamosi Zanzibar na kusema mkutano huo utahudhuliwa na wajumbe wa kundi hilo watakaokuwa hawana dharura.



“Tumekubaliana kwamba siku ya Jumamosi kwa pamoja wajumbe wote ambao hatuna dharula tutaenda Zanzibar kutakuwa na mkutano wa hadhara kuaznia saa nne asubuhi na tutaondoka na siku hiyo na Boti ya saa moja asubuhi kuelekea Zanzibar na katika mkutano huo tutaeleza yaliyojiri katika bunge maalaum.

TAFADHALI ANDIKA MAONI YAKO CHINI HAPA. . .


No comments:

Post a Comment