Tuesday, April 22, 2014

UKAWA WATINGA BUNGENI KUDAI POSHO ZA SIKU AMBAZO HAWAKUHUDHURIA


Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Bungeni, leo wamefika rasmi bungeni na kudai posho, hayo yalisemwa na mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba, linaloendelea mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samweli Sitta alitangaza bungeni jioni hii kuhusiana na tukio hilo ambalo liliwashangaza wabunge wengi waliokuwemo ndani ya bunge hilo.

Mh. Sitta alisema, "Kuna taarifa za kiofisi kuwa UKAWA wamerudi na kwenda kwa mhasibu kusaini posho." Wakati Samwel Sitta anaendelea kutoa maelekezo, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akaomba kutoa taarifa na kutoa ufafanuzi kuwa UKAWA hawastahili kupata malipo yoyote.

Mh. Malima alifafanua kuwa taratibu za posho hizo kwa wale wanao stahili ni waliofanya kazi za bunge pamoja na kuhudhuria vikao vya bunge, hivyo UKAWA hawana ruhusa ya kuchukua fedha hizo mpaka bunge litakaporidhia.

Naye Mh. Doroth Malecela wakati akichangia hoja alimtaka Mwenyekiti wa Bunge hilo kuwataka UKAWA kuingia bungeni na sio kuchukua posho na kutokomea kusikojulikana.

Kundi la UKAWA waliamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge na kuliacha bunge maalumu la katiba linaendela kwa madai ya kutoridhika na mwenendo mzima wa bunge hilo ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi kutoa vitisho kwa wajumbe vinvyolenga kuleta ubaguzi kwa Watanzania.




No comments:

Post a Comment