Tuesday, April 08, 2014

TWITTER KUBADILIKA, ITAFANANA NA FACEBOOK, ANGALIA ITAKAVYOKUWA

Mitchelle Obama ni kati ya wachache kutumia sura mpya ya twitter
Mtandao wa Twitter unazindua rasmi mtandao wake ambapo eneo lake la profile litafanana na Facebook, ambapo itakuwa na picha ya mtumiaji na pia itakuwa kubwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Guardian, toleo hilo jipya litakaloonekana katika sura ya tovuti ya Twitter, itakupa fursa ya kuweka sura unayoitaka, pamoja na tweets, picha kubwa, kurasa pana zaidi, ikifanana na ile ya facebook iliyotengenezwa mwaka 2013.

“tukio kwa tukio, profile yako ya twitter itainesha dunia we ni nani. Kuanzia leo, itakuwa rahisi zaidi (na tunafikiri, raha zaidi) kujieleza kupitia profile mpya ambayo imeimarishwa zaidi” alisema mbunifu wa Twitter, David Bellona alipoandika katika blog.


Watumiaji wataweza ku-zibana twits juu kabisa ya ukurasa wake, wakati zile ambazo zimerudiwa zaidi, kujibiwa na kupendwa zitaonekana kubwa zaidi kidogo.

Waangaliaji wa profile za watu wengine pia wataweza kuchuja muonekano katika sura hiyo bila kuona picha na video au kuona twits na majibu.

Ukurasa mpya wa Profile kwa sasa ni kwa baadhi ya watumiaji waliochaguliwa, ikiwa ni pamoja na watu wachache maarufu, wakati watumiaji wapya wataanza na profile mpya watakapojiunga kwenye vifurushi vyao.

Mfumo huo utaanza rasmi kuanzia wiki zijazo.





No comments:

Post a Comment