Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa anaumia na kuchukizwa na
kitendo cha ongezeko matukio ya dawa za kulevya huku Tanzania ikiwa ndio njia
kwa kutumia viwanja vyake vya ndege vya
kimataifa (JKNI na KIA)kuwa ndio uchochoro.
Rais akizungumza katika hafla ya uzinduzi na kuweka jiwe la
msingi katika uwanja mpya wa ndege ambao utakuwa ni jengo la tatu (terminal 3)
katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JKNI) amemtaka na kumpa mwezi
mmoja Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harison Mwakyembe kufanya kazi na kwamba
hajaridhishwa na utendaji wake.
Alisema kitendo cha watu wanaofanya Biashara ya dawa za
kulevya kuingia na kutoka nchini kirahisi na kwenda kukamatiwa nje ya nchi
kinamuuma na kumkera kwani ni aibu kwake na kwa taifa na inatoa taswira kuwa
wote wanafanya biashara hiyo hivyo amechoshwa na porojo anataka kazi ianze mara
moja.
Rais Kikwete alisema ni wazi uzinduzi wa jengo
hilo la kimataifa utaongeza changamoto kwani utakuwa na idadi kubwa ya watu,
watendaji waelewe kuwa kama hakuna mbinu mbadala ya kudhibiti uingizaji dawa za
kulevya ni tatizo.
“Mna wafanyakazi wachache, hivyo wenye dawa za kulevya
wanapita watakavyo, je jengo hili litakalokuwa na wafanyakazi wengi zaidi na
abiria milioni sita si itakuwa biashara huria!” alisema Rais Kikwete
“tena wanaopita au kukamatwa nasikia wanamuziki, wasanii, au
mkiwaona ndio oya oya piteni. Aibu sana, inaniuma na kuniumiza mno nawambia
haiwezekani ni uzembe”alisema Rais
Aliongeza kuwa afurahishwi na utendaji wa Waziri Mwakyembe
ndio maana anamuuliza kila saa hivyo akikaa na watendaji wake wasinong’one
“Sifurahishwi na utendaji wako Waziri na nyie Mkurugenzi Bw
Suleiman na Mwenyekiti wa Bodi mkielezwa na Waziri muelewe ni maagizo yangu na
yasipotekelezwa nitaanza na nyie hasa we Suleiman” aliongeza kwa msisitizo.
SHUKA CHINI UANDIKE MAONI YAKO...
No comments:
Post a Comment