Tuesday, April 15, 2014

PAPA FRANCIS AOMBA RADHI KWA WATOTO KUDHALILISHWA KINGONO

Ijumaa iliyopita Papa Francis alikaririwa akisema anajisikia kuwajibika kwa vitendo vya kingono walichofanyiwa watoto ambavyo vimelichafua kanisa katoliki, na hivyo kuomba radhi. Papa alitoa tamko hilo alipokutana na NGO (taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusha na watoto wakikatoliki) International Catholic Child Bereu (BICE), alisema:

“Binafsi nawajibika kuchukua dhambi zote zilizofanywa na wachungaji, ni wachache kwa kuwahesabu, ukifananisha na idadi ya wachungaji, ili niombe msamaha kwa uharibifu waliofanya kwa kuwadhalilisha kingono watoto.
Kanisa linaelewa kuhusu uharibifu huo, ni binafsi, uharibifu wa maadili uliofanywa na wanaume wa kanisa, na hatutapiga hatua hata moja kurudi nyuma na kujutia kuhusu tunavyolishughulikia tatizo hili, pamoja na adhabu zinazostahili kuchukuliwa” Papa aliongeza
Papa Francis alisistiza kuwa watoto ni lazima walindwe dhidi ya nia zote mbaya, ikiwa ni pamoja na utumikishwaji, kuingizwa jeshini, na “kuwapa haki ya kukua katika familia yenye baba na mama”

TAFADHALI NDUGU MSOMAJI CHANGIA MAWAZO YAKO HAPA CHINI. . .





No comments:

Post a Comment