Akihojiwa kuhusu taarifa hizi kama ni za kweli au uzushi, mke wa Mzee Yusuph, Leila ‘Malkia’ Rashidi, alisema kuwa ni kweli Mzee Yusuph anastaafu muziki na kwamba hana mpango wa kuendelea na shughuli za muziki kabisa.
“Tunategemea kuzindua albamu mpya na ya mwisho itakayoitwa ‘Chozi la Mama’ na tutaizindua rasmi mwezi juni mwaka huu” alisema Leila alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
Alisema kuwa binafsi amejitahidi sana kumshauri Mzee kuhusu maamuzi yake lakini hakufanikiwa, “marafiki na jamaa mbalimbali pia wamejitahidi lakini tumeshindwa, alichoamua ndio hicho mwenyewe hana mpango tena wa kuendelea na muziki” aliongeza.
Katika albamu hiyo kuna jumla ya nyimbo 6 ambapo ‘Chozi la Mama’ inabeba jina la albamu hiyo na ameimba mwenyewe Mzee Yusuph, nyimbo nyingine ni pamoja na ‘Akiba ya Mapenzi’ aliyoimba Amigo, ‘Fanya Yako’ iliyoimbwa na mke wa Mzee Yusuph, Malkia Leila Rashid.
Alipoulizwa nini sasa itakuwa hatma ya wanamuziki wa bendi hiyo, Leila alisema, “ndio watatafuta bendi za kwenda au kazi za kufanya, lakini mwisho ni juni mwaka huu katika albamu yetu ya mwisho.”
“Najua wapenzi wetu wengi watashtushwa na kuguswa wakisikia jambo hilo, lakini wako wengine wengi tu watakaofurahishwa pia” aliongeza Leila
Leila alisema kuwa hatma ya Mzee mwenyewe itakuwa ni kuingia katika shughuli za kisaisa na kujiendeleza huko. Aidha Leila anasema Mzee amejiandaa kwa kufungua miradi mbalimbali ambayo itatusaidia kuendesha familia pamoja na kusomesha watoto.
Leila alisema kuwa hatma ya Mzee mwenyewe itakuwa ni kuingia katika shughuli za kisaisa na kujiendeleza huko. Aidha Leila anasema Mzee amejiandaa kwa kufungua miradi mbalimbali ambayo itatusaidia kuendesha familia pamoja na kusomesha watoto.
Inadaiwa kuwa Mzee Yusuph anajiandaa kwenda kugombea ubunge Zanzibar, ila haijulikani atagombea jimbo gani.
Nyimbo nyingine katika albamu hiyo ni pamoja na ‘Asidi Hana Sababu’ nyimbo iliyoimbwa dada yake Mzee Yusuph, Hadija Yusuph, nyingine ni ‘Asiye na Kasoro ni Mungu’ iliyoimbwa na Fatma Mcharuko na ya mwisho ni ‘Aliyepanga Ni Jalali ‘ iliyoimbwa na Mwasiti ‘Sauti ya Kasuku’ Mbwana.
Malkia Leila naye alisema hana mpango wa kuendelea na shughuli zozote za muziki, “namuombea mafanikio kwa mungu ili mambo yasiyumbe” alimaliza Malkia Leila
TAFADHALI ANDIKA MAONI YAKO HAPA CHINI KUHUSIANA NA STORY HII. . .
No comments:
Post a Comment