Tuesday, April 29, 2014

MUSIC: JHIKOMAN AENDELEA KUFANYA MAAJABU UGHAIBUNI, ANGALIA VIDEO HAPA

Mwanamuziki mashuhuri wa reggae barani Afrika, Jhikoman & Afrikabisa Band toka Bagamoyo, mkoa wa Pwani, Tanzania anarajiwa kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa watakao tingisha onesho kubwa la 5 la kimataifa lijulikanalo kama International African Festival-Tubingen linalotarajiwa kufanyika mjini Tubingen, nchini Ujerumani Kusini kuanzia 17 Julai mpaka 20 Julai 2014.

Mwanamuziki huyo nyota Jhikoman kwa sasa yuko nchini Finland ambapo anafanya maonesho katika majukwaa ya kimataifa na kabla ya kuelekea nchini Norway na kwingineko. 

Video chini ni kionjo tu cha kazi ya Jhikoman inayoendelea. . .
No comments:

Post a Comment