Tuesday, April 08, 2014

MAJAMBAZI YATEKA MAGARI YA MAGAZETI, YAFANYA UNYAMA

Iringa

Watu wanasadikiwa kuwa ni majambazi ambayo idadi yao haikufahamika mara moja usiku wa juzi wamefunga barabara ya Morogoro -Iringa eneo la Doma na kufanya unyama wa kutisha kwa wasafiri wa barabara hiyo ikiwa ni pamoja na kuwalazimisha kufanya mapenzi wanaume kwa wanaume na kuwatesa vibaya madereva kabla ya kuwapora mali zao.

Miongoni mwa walioteswa ni pamoja na Rasta ambaye ni dereva wa gari la magazeti ya kampuni ya Global Publishers ambae inadaiwa amejeruhiwa mkono huku dereva wa gari la magazeti ya kampuni ya Mwananchi akinusurika na gari lake kupinduka wakati akikwepa vizuizi vya magogo vilivyotegwa barabarani.
Wakizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya jana mjini Iringa wahanga wa tukio hilo Ally Malinda (44) mkazi wa Kitunda, Dar es Salaam na Rashid Yusuph Kahese (37) mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam ambao kwa pamoja wanaendesha gari ya magazeti ya kampuni ya The Guardian walisema kuwa tukio hilo lilitokea muda wa saa 8 usiku wa jana hadi saa 11 alfajiri baada ya watekaji hao kuachia mateka hao.
Malinda alisema kuwa kabla ya kufika eneo ambalo watekaji hao walikuwa wamewateka abiria wengi zaidi walikua na makundi ya watu waliotekwa na kuporwa ambao walikuwa wakiwasimamisha wasiendeleena safari ila hawakusimama wakijua ni wezi .

Anasema kuwa walienda mbele kidogo na kakutana na kundi jingine ambapo hawakukata tamaa na kupuuzia na kupita ila baada ya kufika mbele ndipo walipoona magari yakiwa yamegeuka huku na kule, huku wengine wakiteswa na ndipo walipofanikiwa kugeuza gari lao lenye namba za usajili T 812 CNZ na kukimbia .

Hata hivyo alisema polisi Morogoro walipigiwa simu ila hawakuweza kufika hadi majira ya saa 11 Alfajiri watekaji hao walipoamua kuwaachia mateka.

" Kila tukimpigia kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro aliishia kusema kuna askari wametumwa kuja eneo la tukio ila hadi asubuhi hakuna askari aliyefika .....na majeruhi wamepelekwa Hospital ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi"


No comments:

Post a Comment