Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa tarehe
ijumaa(25/04/2014) kwenye mtandao wa Metro, Nou Nou alipatwa tatizo hilo ambalo
linaendelea kukua ambalo husababishwa na
kutokea kwa nafasi katika uti wa mgongo. Katika kipindi cha siku tano baada ya
kuzaliwa mama yake aligundua kamkia kanaanza kuota na sasa mtoto huyo ana mkia
unaoonekana kabisa.
Akiwa na wasi wasi kuhusu makuzi ya mtoto wake, mama yake
Nou Nou amewaomba wapasuaji katika hospitali ya Changsha nchini China, kutafuta
namna ya kuondoa mkia huo.
Hata hiyvo madaktari hao wanasema hakuna wanachoweza kufanya
kwani mkia huo umeungana na mishipa ya fahamu, na kama wakiondoa atapata kilema
cha maisha. Tatizo hilo hutokea mara chache na kumpata mtu mmoja kati ya watu
1000. Lakini pia kutokea ni nadra sana na hasa kukua kwa mkia kama huo.
TAFADHALI SHUKA CHINI UANDIKE MAONI YAKO. . .
No comments:
Post a Comment