Thursday, April 24, 2014

KOCHA WA SIMBA ANAONDOKA LEO USIKU, SOMA HAPA KUJUA HATMA YAKE

Kocha Mkuu wa Simba Zdravko Logarusic (kulia) anaondoka leo saa tatu usiku nchini kurudi kwao kwaajili ya mapumziko nyumbani kwao Croatia .

Akiwa katika maandalizi ya safari yake, imedhibitishwa kwamba atarudi nchini kuendela na kandarasi ya kuifundisha Simba baada ya kusaini mkataba. Zakaria Hans Pop, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba amedhibitisha kuongea na Locarustic kuhusiana na  hatma yake katika klabu hiyo kongwe ya soka nchini.

Zdravko Logarusic ambaye alikuja mwaka 2013 na kushika mikoba ya Simba wekundu wa Msimbazi baada ya kuchukua nafasi hiyo toka kwa Abdalah Kibaden
amemaliza msimu wa ligi mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Simba ilikwaana na watani wao wa jadi Yanga, katika mechi ya kumaliza mzunguko wa ligi ya Vodacom (VPL) na kuibuka na sare ya 1 -1.

Akizungumza na Imma Matukio, Bw.Pop alisema kuwa Logarusic amekabidhiwa mkataba ambao bado hajasaini, lakini anatarajiwa kusaini atakaporudi baada ya mapumziko yake.


“Tumempa mkataba wa mwaka mmoja na tunategemea atasaini atakaporudi baada ya mapumziko yake” alisema Hans Pop. Zdravko Logarusic anatarajiwa kupumzika kwa muda wa mwezi mmoja kabla hajarudi kutoka nyumbani kwao.
TAFADHALI SHUKA CHINI KUWEKA MAONI YAKO. . .

No comments:

Post a Comment