Sunday, April 27, 2014

KIPA WA COASTAL UNION HAITAKI TENA TIMU HIYO

Kipa Shaaban Hassan Kado wa Coastal Union amesema hataoongeza mkataba tena wa kuchezea time hiyo ya Tanga baada ya kumalizika msimu huu na anafungua milango kwa timu nyingine zinazo muhitaji kufanya naye mazungumzo.

Akizungumza na mwandishi wetu jana mjini Dar es Salaam, Kado amesema kwamba hataki kusema mengi kuhusu time yake ya Coastal Union , ila anashukuru kwa misimu miwili aliyokuwa na timu hiyo na anaachana nayo.

Jambo zuri kwa Kado ni kwamba anatarajia kufungua plasta gumu (PoP) Mei 5 katika mkono wake wa kushoto na moja kwa moja kuanza mazoezi. Kado aliumia katika mchezo dhidi ya Ashanti United Machi mwaka huu na mbaya zaidi akatelekezwa na uongozi wa Coastal hivyo kulazimika kujitibu kwa gharama zake mwenyewe.

Kipa huyo wa zamani wa Moro United, Mtibwa Sugar zote za Morogoro na Yanga ya Dar es Salaam, amesema timu yoyote inayomuhitaji imsake kwa mazungumzo. “Nasema mimi kwa sasa ni mchezaji huru na ninaendelea na mazoezi kwa sababu niliumia kiganja cha mkono, ila mazoezi ya kudaka nitaanza kuanzia Mei 10,”alisema Kado ambaye amechezea timu ya taifa, Taifa Stars pia.

TAFADHALI SHUKA CHINI UANDIKE MAONI YAKO. . .


No comments:

Post a Comment